Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuwalinde watoto na unyanyasaji wa kingono mtandaoni

Muktasari:

Picha na video zenye maudhui haya huweza kuripotiwa na mtu yeyote kwa kutumia tovuti maalumu.

Mwaka 2018 zilipatikana takribani tovuti 105,000 zenye maudhui ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto.

Tovuti hizi huwa na picha na video nyingi zinazoonesha watoto wakifanyiwa unyanyasaji kingono na kwa mwaka jana peke yake, zaidi ya picha 340,000 zilipatikana katika tovuti hizi na kuondolewa mtandaoni.

Takwimu hizi zinatokana na ripoti ya Internet Watch Foundation, shirika linalofanya kazi ya kutafuta na kuondoa maudhui yoyote ya unyanyasaji wa watoto kingono yaliyopo mtandaoni.

Picha na video zenye maudhui haya huweza kuripotiwa na mtu yeyote kwa kutumia tovuti maalumu.

Tatizo la kuwepo na kutumika kwa picha za unyanyasaji wa kingono kwa watoto limeenea zaidi katika nchi zilizoendelea kuliko nchi zinazoendelea lakini tatizo hili lipo hata hapa nchini.

Ndani ya miezi mitatu ya mwaka 2019, tovuti inayopokea taarifa za maudhui ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto yanayowekwa mitandaoni imepokea taarifa 3 za unyanyasaji huu kutoka Tanzania na kuondoa maudhui haya.

Ni faraja kufahamu kwamba kumbe tunapokutana na picha zenye kuonesha watoto wakifanyiwa unyanyasaji wa kingono mtandaoni, tunaweza kuwasaidia kwa kutoa taarifa na picha hizi zikaondolewa.

Lakini hii haitoshi kuwalinda watoto, ni jukumu letu kuhakikisha tunawalinda watoto kwa kuepuka maudhui haya kuwepo mitandaoni na katika vifaa vyetu vya kielektroniki.

Fanya mambo yafuatayo ili kumlinda mwanao na watoto wengine dhidi ya maudhui ya kuwanyanyasa watoto kingono mtandaoni. Mosi; epuka kumpiga mtoto picha akiwa mtupu Ð awe wako ama wa mtu mwingine.

Pamoja na kwamba tunapenda kuweka kumbukumbu za wanetu kadri wanavyokuwa, ni muhimu tujaribu kuweka mipaka ya kumbukumbu tunazohifadhi katika vifaa vya kielektroniki.

Huwezi jua nani atachukua na kuona picha hizi kama ana nia njema na mwanao ama la usimpe kisingizio. Lakini vilevile, kabla ya kumpiga mwanao picha akiwa mtupu jiulize, ‘Je, baada ya miaka kumi, ataipenda picha hii ama itamfedhehesha na kumfanya asikie aibu?

Je, utajisikiaje picha hii ikisambaa kwa bahati mbaya?’ Kumbukumbu nyingine tujitahidi kuzihifadhi katika mioyo yetu. Pili; usisambaze picha za unyanyasaji wa kingono kwa watoto hata kwa minajili ya kuwaonya wazazi ama kuelimisha jamii.

Mara nyingi tumeona picha na video za watoto wakifanyiwa ama kuhojiwa kuhusu unyanyasaji wa kingono zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kama WhatsApp, Facebook na Instagram.

Unapopokea picha ama video ya mtoto akifanyiwa unyanyasaji wa kingono, mlinde kwa kuifuta kabisa na kisha waelimishe na wengine waifute ili isisambae zaidi.

Hata kama unataka kuwapa angalizo wazazi wengine kuhusu unyanyasaji wa kingono unaoweza kuwakuta watoto wao, tafakari kwanza, Ingekuwa picha ya mwanao, ungefurahia kuiona ikisambaa kama angalizo kwa wazazi wengine?