Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Unapochagua mchumba yazingatie yafuatayo

Kuoa au kuolewa, kama wasemavyo siku hizi, si suala la kukurupuka au kununua tiketi ya bahati nasibu.

Katika kuchagua mwenza wako unapaswa uwe makini, usikurupuke kuamua kuingia kwenye uhusiano, mara zote huwa na mwanzo lakini hauna mwisho, labda mtenganishwe na kifo kwa wale waumini wa dini ya Kikristo.

Hivyo, ni muhimu kumjua mwenzako kwa udhaifu na ubora wake. Lazima uwe na orodha ya vitu unavyopenda mwenza wako awe navyo kama vile umri, atokako, tabia, urefu, uwezo wa kufikiri, mvuto, mengine mengi kulingana na utakavyo. Kama ilivyo kwenye kujenga nyumba au kununua gari, lazima ujue ukubwa hata muundo wa nyumba. Kama ni gari, ungependa kujua aina, ulaji wake mafuta, rangi, mwaka wa kutengenezwa na hata ubora na udhaifu wake.

Kwa vile ndoa ni taasisi unayoingia kwa sababu za upendo na uhuru wa kuchagua, siyo sawa na kuzaa watoto au kuzaliwa. Wazazi hawachagui watoto wala watoto hawachagui wazazi kwa sababu hawana uwezo wa kufanya hivyo. Kwa upande wa ndoa, una chaguo huru ambalo likishafanyika, huondoa uhuru huo. Hivyo, unapaswa kuwa makini, mvumilivu na mwerevu kufikia kusema ndiyo.

Hivyo, tofautisha kumchagua rafiki mnayeweza kufarakana na kuamua kuvunja urafiki. Ndoa ni zaidi ya urafiki, maana, rafiki hana haki kisheria kumrithi au kumrithisha rafiki yake mali zake pale inapotokea kafariki dunia.

Tofauti, mwanandoa anakuwa na haki hata zaidi ya wazazi na ndugu kwenye kukumiliki wewe na mali zako. Hivyo, huyu si mtu wa mchezo. Hakuna anayefunga ndoa akitegemea kuna siku itavunjika, japo nyingi zinavunjika.

Katika mila za Kiafrika, ndoa huwahusisha wazazi, ndugu, na jamaa katika kuanza kuijenga, hata wakati mwingine kuibomoa na hufanya familia mbili tofauti kuwa moja.

Familia mbili huhusisha familia nyingine nyingi ambazo hazikuhusiana kabla kuingia katika uhusiano usio na mwisho japo una mwanzo.

Ndiyo maana tuna washenga, makuwadi, na wengine wengi tunaowahusisha kwenye kuanza msingi wa ndoa ambao, kimsingi, ni watu wa karibu na wanaoaminika walio karibu nawe kwa uhusiano wa damu ambao, mara nyingi, huteuliwa na wazazi wetu kutokana na ukaribu na imani yao kwao. Hii ni kutokana na wahusika kuwa na uzoefu wa muda mrefu, mbali na ujuzi ambao huchukua miaka mingi kuupata.

Tunadhani utaratibu huu ndio uliowawezesha wazazi na mababu na mabibi zetu kutokuwa na talaka, kwani ulikuwa siyo shirikishi tu, bali wenye umakini zaidi katika kutafuta wahusika wanaofaa na kufaana kutokana na walivyowajua.

Kwa Waafrika, hata neno talaka ni la kigeni litokanalo na lugha ya Kiarabu iliyoleta Uislamu. Kabla ya hapo, hatujui dhana hii ilivyotafsiriwa. Japo talaka zinatolewa, huwa si jambo la kufurahisha wala kutamani liwepo, ukiachia mbali kwenye zile ndoa ambazo ni rahisi kuoa na kuacha kulingana na misingi na taratibu zilizojiwekea.

Kumalizia, bila kuzama zaidi kwenye mada kutokana na ufinyu wa nafasi, wanyama hawana ‘send off’, vyeti vya ndoa wala mikataba inayojulikana kwa binadamu, wana dalili zinazoashiria thamani ya ndoa. Hii ni elimu mwanadamu aliyoipata kutoka kwa mwalimu mchwa. Kama tukubalivyo kupata ujuzi huu toka kwa mwalimu huyu, kadhalika tukubali na ukweli juu ya taasisi hii ya ndoa kutoka kwa viumbe mbalimbali waliotuzunguka.