Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fani katika tamthiliya ya Orodha

Muktasari:

Kimaudhui, msanii amefaulu kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa wa ukimwi. Anaonyesha kuwa ugonjwa huu ni hatari na hutokana na kufanya ngono, huku matokeo yake yakiwa ni kifo.

Misemo/nahau

Hizi ni tungo ambazo maana yake halisi ni tofauti na maana ya kawaida ya maneno husika. Kwa mfano, Baba Furaha anapomwambia mwanae Furaha, “Unachohitaji ni mkono wangu pengine” Baba Furaha alikua anonyesha ghadhabu yake juu ya Furaha.

 

Taswira

Haya ni maneno yanayoundwa na mwandishi ili kuleta picha ya kitu fulani akilini au katika fikra za msomaji au msikilizaji wa kazi za fasihi. Katika tamthiya hii taswira zifuatazo zimetumika.

Ua kavu: Kwa maana ya msichana mzuri aliyeteketea kiafya. Hapa msanii alikua akimzungumzia Furaha ambaye alikuwa mrembo lakini maradhi ya ukimwi yakapoteza kabisa ule uzuri wake.

Mbu wadogo: Kwa maana ya watoto wadogo ambao wanategemea wazazi wao . Bado wananyonya, yaani bado wanawategemea katika maisha yao.Furaha anawategemea/anamtegemea mzazi wake katika maisha yake.

Punda: Furaha alifananishwa na punda wa kijiji yaani mwanamke aliyelala na wanaume ovyo. Mwandishi anasema yeyote aliyemtaka Furaha alimpata.

 

Mandhari

Ni sehemu amabayo kazi ya fasihi hufanyika. Katika tamthiliya hii mandhari ya tamthiliya hii ni,barabarani,baa ya kienyeji, kanisani, nyumbani kwao Furaha na Makaburini.

 

Jina la kitabu

Jina la kitabu ni Orodha. Orodha ni mlolongo wa vitu. Katika tamthiliya hii Orodha inakusaidia mambo ya msingi yanayoweza kuepusha mtu kupata virusi vya Ukimwi.

Jina la kitabu linaendana na yaliyomo ndani ya kitabu hicho. Mwandishi anaonyesha orodha ya vitu kama uelewa, uwazi na ukweli, upendo vikikosekana ndicho chanzo cha maambukizi dhidi ya ugonjwa wa ukimwi. Orodha inajitokeza katika sura tofauti pia ambapo wanakiji wanataja majina ya watu waliotembea na Furaha. Kwa mfano, Bw.Ecko, BwJuma, Salim na Kitunda.

Kufaulu na kutofaulu kwa mwandishi

Kimaudhui, msanii amefaulu kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa wa ukimwi. Anaonyesha kuwa ugonjwa huu ni hatari na hutokana na kufanya ngono, huku matokeo yake yakiwa ni kifo.

Mwandishi amefaulu kuielimisha jamii juu ya njia mbalimbali za kitalaamu zinazoweza kutumika kuzuia ugonjwa hatari wa ukimwi. Njia hizo ni pamoja na wenza kuwa wakweli, waadilifu na nyinginezo.

Katika sura nyingine, mwandishi ameweza kuonyesha imani potofu walizonazo wananchi hasa wa kijijini. Wapo wanaodhani kuwa ugonjwa wa Ukimwi unaenezwa kwa kugusana na mtu aliyeathirika au wengine kuamini kuwa ugonjwa huo hupatikana kwa kulogwa.

Kwa upande wa fani, mwandishi amefaulu kuchora wahusika wake kwa kuonyesha wasifu wao katika uchangiaji wa ugonjwa wa ukimwi. Wahusika wa tamthiliya hii ni wa rika tofouti. Rika hizi huwa na uhusiano wa kimapenzi kiasi cha kuwafanya waambukizane ugonjwa wa ukimwi.

Kwa upande mwingine msanii amefaulu kutumia mandhari ya kijijini kama sehemu muhimu iliyoathirika zaidi na ugonjwa wa ukimwi. Hii inatokana na elimu duni waliyonayo wanakijiji. Huu ni uhalisia wa vijiji vingi hapa Tanzania. Furaha ni mwanakijiji aliyeathirika kutokana na ukosefu wa elimu ya kijinsia.

 

Kwa upande wa lugha, mwandishi amefaulu kutumia lugha ya kawaida na inayoeleweka. Kumtumia mhusika kama Kituda ni mafanikio makubwa kwani amezungumza lugha ya mtaani ambayo hupendwa na vijana wengi.