Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msimu mwingine wa furaha ya familia, fursa kwa wajasiriamali Sabasaba

Muktasari:

  • Baada ya maandalizi ya siku nyingiyatakayokata kiu ya Watanzania kwa michezo ya watoto huku wazazi wao wakipata nafasi ya kununua bidha za aina tofauti, Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (DITF 42) maarufu kama Sabasaba yanaanza leo na yataendelea mpaka Julai 13.

Ni msimu mwingine wa familia kufurahi, kampuni na wajasiriamali kubadilishana mawasiliano ya kuimarisha biashara kwenye Maonyesho ya Sabasaba mwaka huu.

Baada ya maandalizi ya siku nyingiyatakayokata kiu ya Watanzania kwa michezo ya watoto huku wazazi wao wakipata nafasi ya kununua bidha za aina tofauti, Maonyesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (DITF 42) maarufu kama Sabasaba yanaanza leo na yataendelea mpaka Julai 13.

Maelfu ya wananchi wanatarajiwa kutembelea Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere yanakofanyika yakishirikisha nchi 32.

Nchi mbili zimeongezeka mwaka huu zikilinganishwa na zilizoshiriki mwaka 2017 zilizowakilishwa na kampuni 500 za kigeni. Kati ya nchi hizo 32 zitakazowakilishwa mwaka huu, tano zitashiriki maonyesho hayo kwa mara ya kwanza zikiwa na teknolojia mpya na ya kisasa.

Nchi hizo ni Australia, Marekani, Ufilipino, Morocco na Cuba. Watakaohudhuria maonyesho hayo mwaka huu watapata fursa ya kukutana wageni wengi zaidi kwani zaidi ya washiriki 2,000 wa ndani wamethibitisha kuwapo. Maandalizi Kabla watembeleaji wa maonyesho hayo hawajaanza kupata wanachokitarajia kundi la kwanza limeshanza kunufaika.

Hawa ni vijana wanaojitafutia chochote kwenye maandalizi ya kampuni zinazoshiriki. Kwa wiki mbili zilizopita, Mwananchi limeshuhudia vijana wengi wakipamba mabanda na kuyapaka rangi ili kuongeza mvuto kwa wateja watakaokupata wasaa wa kuyatembelea.

Taarifa za Mamlaka ya Mendeleo ya Biashara (Tantrade) inayoratibu na kusimamia maonyesho hayo zinaonyesha ongezeko la washiriki kila mwaka jambo linalomaanisha fursa za ajira za muda mfupi kwa vijana wanaochangamka

Mwaka 2016, takwimu za Tantrade zinaonyesha kulikuwa na washiriki 2,000 ambao waliongezeka mpaka 2,500 mwaka jana huku kampuni za nje ziliongezeka kutoka 500 hadi 515.

Meneja ukuzaji biashara wa Tantrade, Stephen Koberou anasema mwaka huu kutakuwa na matukio mengi zaidi ikiwemo siku maalumu ya kuzikutanisha biashara (B2B) za ndani na nje ili kubadilishana uzoefu.

Anasema elimu ya masuala tofauti itatolewa hivyo kuwataka wananchi kushiriki kikamilifu siku maalum ya kupinga rushwa, kliniki ya biashara, ardhi na mendeleo ya viwanda, utalii na viwanda, wanawake na maendeleo ya viwanda, sanaa na utamaduni, mazingira na vijana.

Kuongeza ladha zaidi, Koberou anasema maonyesho ya mwaka huu yatadumu kwa siku 16 kutii agizo la Rais John Magufuli alilolitoa mwaka jana wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya 41 kwa lengo la kuwapa wananchi elimu ya masuala mbalimbali ya uwekezaji na biashara.

“Wadau wote wanakaribishwa kushiriki katika siku hizo muhimu kwani watapata fursa ya kujifunza mambo mengi mfano hilo ya rushwa, kutakuwa na watalaamu wakitoa mada,” anasema meneja huyo.

Kwenye mikutano ya kubadilishana uzoefu baina ya kampuni, anasema mwaka huu kutakuwa na fursa ya wadau wa sekta ya maziwa, bidhaa za matunda na mbogamboga, kuku na mafuta ya alizeti kukutana na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili ilikutafuta suluhisho la kudumu.

Kuhusu fursa kwa wajasiriamali, meneja huyo anabainisha kuwa kutakuwa na teknolojia mpya kutoka vyuo vya ufundi zinazosaidia kuendesha viwanda vidogo.

Gharama

Hakutakuwa na mabadiliko makubwa ya gharama za kutembelea maonyesho hayo mwaka huu. Kiingilio kwa siku za kawaida wakubwa watalipa Sh3,000 wakati watoto wakitozwa Sh1,000. Siku ya Sabasaba yenyewe, wakubwa watalipa Sh4,000 ili kujionea na kutembelea mabanda tofauti huku watoto wakiendelea kiingilio kilekile.

Kwa watakaoenda na magari watalipa tozo ya maegesho kiasi cha Sh10,000 kwa kiwango ambacho ni sawa na kilichokuwapo mwaka jana.

Vitambulisho vya waonyeshaji na vingilio getini vinaratibiwa na kitengo cha kampyuta cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambachoo kimeshakamilisha maandalizi kwa kiasi kikubwa na kutoa ajira kwa vijana.

Baada ya Tantrade kuwapata vijana wa kutosha watakaokuwa wakitoa vitambulisho na kuuza tiketi za kuingilia kwenye viwanja hivyo, baadhi ya wafanyabiashara walianza kuingiza bidhaa zao na kuzipanga.

Wakati wa maandalizi hayo, gazeti hili liliwashushudia wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakijitolea kupanga viti kwenye baadhi ya mabanda ya vyakula na kupaka rangi kuta.

Mmoja wa wanafunzi hao kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Emmanuel Mgelwa alikutwa ofisi za Tantrade akiomba kazi ya kuokota karatasi zilizotumika.

Mgelwa anasema ana kampuni yake inayojishughulisha na uokotaji karatasi katika ofisi mbalimbali hivyo amekuja Sabasaba kuomba kujitolea kuokota zilizopo na kusaidia kuweka mazingira katika hali ya usafi.

“Huwa tunaokota kisha tunaenda kuziuza katika viwanda vya kutengeneza karatasi, tumeona tuje hapa kuona kama tunaweza kupata za kutosha,” amesema.

Mbali na Mgelwa, wapo wanafunzi wengine wenye ujuzi wa fani nyingi nyingine ambao wameenda kuomba kufanya kazi za muda mfupi kwenye maonyesho hayo.

Mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), Jenifa Josepha anasema: “Maonyesho ya Sabasaba yamekuwa na manufaa makubwa kwa wanafunzi kwani wengi tunakuwa likizo hivyo inatupa fursa ya kuomba kazi za muda.”

Anasema ni mara ya pili kwake kushiriki maonyesho hayo. anaeleza kuwa mwaka jana alipata kazi na alikuwa akilipwa Sh30,000 kwa siku fedha ambayo ilimsaidia kwenye matumizi yake madogo madogo.

“Mwaka huu vijana wa chuo wamejitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hii kwa hiyo sijui kama nitapata, ngoja tuone,” anasema.

Ofisa mwandamizi wa kitengo cha habari wa Tantrade, Theresa Chilambo anasema wanapokea maombi mengi kutoka kwa wanafunzi wa chuo kwa ajili ya ajira za muda.

“Kila mwaka huwa tunatoa ajira za muda kwa vijana wenye taaluma mbalimbali na baadhi ya washirki wakihitaji wafanyakazi huwa tunawapatia. Monyesho haya yana fursa nyingi ya vijana kujipatia kipato,” anabainisha.

Aidha, anaomba wananchi wa Dar es Salaam na mikoa mingine kujitokeza kwa wingi kushiriki maonyesho ya mwaka huu kwani yamesheheni vitu vingi vitakavyokata kiu kuanzia ya watoto mpaka watu wazima ikiwamo tekinolojia za kisasa kurahisisha mambo mbalimbali.

Usalama, mapato

Kuhusu usalama Theresa anasema limepewa kipaumbele cha juu kwani kutakuwa na kamera maalum kila banda kuhakikisha mali za washiriki zinakuwa salama sambamba na kuwabana wezi wote watakaojaribu kuiba.

Hivi karibuni mkurugenzi mkuu wa Tantrade, Edwin Rutageruka alisema mwaka huu wanatarajia mapato yataongezeka kwa asilimia 70 baada ya kufunga mfumo wa Teeknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Mkurugenzi huyo anasema mwaka jana mamlaka hiyo ilipata asilimia 46 zaidi ya mapato iliyopata mwaka 2016 ongezeko lililochangiwa na kazi nzuri iliyofanywa na UDSM kuhakikisha kila kitu kinakwenda kidijitali.

“Tunawashukuru sana chuo kikuu kwani walifanya kazi iliyotukuka na mwaka huu tunatarajia mapato zaidi kwani mfumo wao uko wazi na tunaona kila kinachoendelea,” anasema.

Licha ya kuimarika kwa mapato hayo, mwaka jana mamlaka hiyo ilifanikiwa kuunganisha biashara zenye thamani ya Sh15 milioni kupitia mikutano ya wafanyabiashara (B2B) na kuahidi kuongeza idadi na thamani ya mikataba itakayoafikiwa mwaka huu kwa kuongeza idadi ya mikutano.