Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NDANI YA BOKSI: Mpeni ‘breki’ kidogo Paula wa Kajala...

Paula. Yes mtoto wa P Funk Majani. Yes mtoto wa Kajala Masanja. Viumbe wawili wenye mizuka ya sanaa. Mmoja mchizi muziki mwingine mchizi filamu. Kwa pamoja waliunganisha damu na kumpata Paula. Achana na

Kajala huyu mwenye akili za Bongo Movie. Uliza watu Kajala wa Jiteute na mitaa ya ‘Obey Polisi’. Wakati huo rangi yake haijaongezwa ‘bando la wiki’.

Alikuwa mfano halisi wa mtoto wa kike wa Kiafrika. Mzuri mpaka anakera. Madogo kibao wamekula vitasa vya kutosha kwa P Funk pale Bamaga. Hakutaka ulete mazoea na ‘tunda lake la Kisukuma’. Ukienda kurekodi kwa Majani fuata kilichokuleta. Ukitaka kumzoea Kajala lazima utandikwe na nyimbo utarekodia kwa bibi yako.

Wivu wa Majani kwa Kajala hakuna mwanaume aliyeshangaa. Hata wewe

ungeleta wivu kama Majani. Mtoto mteke kama maini. Kichwani nywele

fupifupi zenye kuvutia kuliko posho za Bungeni. Kajala yule ningeambiwa nichague ajira ya umoja wa mataifa au nimmiliki yeye. Bila ajizi wala kusita siyo tu ningeikataa ajira ningewashitaki kwa kumfananisha Kajala na vitu vya kijinga.

Kama marehemu Ndikumana alivyochanganywa na ‘mwili rojorojo’ wa Irene Uwoya. Ndivyo ambavyo Majani alikuwa kama ‘Zuzu la Wiki’ mbele ya Kajala. Hakuwa msanii wakati huo. Wala hakushiriki Miss Bantu ingawa alistahili. Lakini alikuwa staa mwenye ustaa wake tangu anasoma Jitegemee. Majani akasema “msinichezee’’. Akamficha jumla.

Pale studio kwa Majani Bamaga. Ilikuwa rahisi kusikiliza ‘biti’ au kurekodi kuliko kumuona Kajala. Alilindwa na kuhifadhiwa kama Malkia wa Sheba. Wasanii waliomfahamu kabla aliwavutia kuliko ‘biti’ za Majani. Yaani ilikuwa raha kumtazama Kajala kuliko kusikiliza makelele ya midundo studio pale. Nielewe… Kajala huyu na yule, yule alikuwa bora zaidi.

Maendeleo yameondoka na rangi adimu ya Kajala. Rangi ile iliyofanana na mbao ya mninga imetoweshwa kikatili. Alikuwa na rangi ya ‘chocolate’ haswa. Alikuwa zaidi ya utundu wa ‘filta’ za instagram wanazokoleza madem wa mjini.

Unamjua Kajala unamsikia. Achana na miyeyusho ya biashara ya muziki. Penzi la Kajala lilipoota mbawa kikawa chanzo kikuu zaidi cha Majani kususa ‘gemu’. Mimi siyo tu ningesusa ‘gemu’ pia ningeenda kuishi kwa

‘Mshua’ Uholanzi. Bora kuachwa na basi la mshahara kuliko kutengwa na mwili na sura ya Kajala yule. ‘Ene wei’ siyo rangi ya Kajala tu. Maendeleo yameondoa vitu vingi.

Kila shirika nchini au idara yoyote ilikuwa na bendi ya muziki.

Uhamiaji. Bima. DDC. Tancat Almasi. JKT. Jeshi la Polisi na mashirika na taasisi nyingi zilimiliki bendi. Hivi sasa siyo tu hakuna bendi hata mashirika yenyewe mengi yametoweka kama Kisonono. Dunia imebadilika sana.

Wazee wetu waliburudishwa na muziki mwishoni mwa juma. Wanamuziki waliajiriwa kama wafanyakazi wengine kwenye shirika au taasisi husika.

Maisha yalikuwa safi. Ndiyo maana wazee wengi wamejenga nyumba zao ingawa hawakutengeneza pesa kama Mr Nice. Muziki ilikuwa ajira rasmi.

Leo hii muziki siyo tu ajira bali ni biashara kubwa.

Bendi za mashirika zilikufa kama mashirika yenyewe. Zikabaki bendi za watu binafsi. Nazo hivi sasa zimekufa ingawa mazishi bado kufanyika.

Tunamsikia Christian Bella tu naye kama msanii binafsi siyo kiongozi wa Malaika Band. Hata muziki wa kizazi kipya nao makundi yametoweka. Hakuna Wanaume Family wala East Coast Team. Wamebaki wasanii binafsi ambao nao siyo wengi kwa kiwango kile. Mwaka unaenda wa 10 huu mastaa halisi wanabaki kuwa wawili tu Diamond na Alikiba. Huwezi kusema muziki unakua kwa mtindo huu. Wengine wanaishia kuwa wasindikizaji mpaka kimafanikio.

Ndiyo maana hata wasanii wa kuigiza hawaeleweki hii leo. Walianza na tamthilia, wakaingia kwenye filamu sasa wamerudi kwenye tamthilia. Na siyo kikazi. Hapana, wamerudi kama mashabiki.

Nao wamekuwa mashabiki kama mashabiki wa tamthilia ya Sultan na Wakorea. Wanaoneemeka ni wale wa mitaani wanaotafsiri kihunihuni filamu za wazungu na kuingiza kiswahili chao cha kibwege.

Wanaingiza mkwanja kuliko Jb. Kiswahili hawawezi, kwenye L wanaweka R. Tamthilia wanatamka tamsilia.

Hili Basata hawalioni kama tatizo kwa soko la wasanii wetu wa ndani.

Wao wako ‘bize’ kusubiri Diamond aimbe matusi wamfungie. Ney wa Mitego na Nikki Mbishi watoe ngoma za kuongelea ‘ishu’ za watawala wawafungie.

Ulezi kwa sanaa na wasanii wameweka kando na kujikita kusimamia maadili tu kama waalimu wa nidhamu mashuleni. Basata huenda ndo kitu pekee kinachodaiwa na sanaa na wasanii kuliko kitu chochote. Wanasubiri wasanii wakosee badala ya kuwaongoza wasikosee.

Ni kutotambua kama sanaa ni biashara kubwa kuliko korosho. Wasanii wanajiongoza kiyatima. Hawajui kesho yao. Sanaa inajiendesha kama kuku aliyechinjwa shingo. Kifupi ni kwamba wakati ule wa Mwalimu Julius sanaa ilithaminiwa. Haya maendeleo yamekuja na kuondoa hata utamu wa ngoma za Moris Nyunyusa kwenye taarifa ya habari RTD. TBC nao wanataka kusikika ‘kisienieni’.

Watoto wametekwa na utandawazi. Wako makini kujifunza utumiaji wa simu janja kuliko uvaaji wa magaguro. Wanajua kufuga kucha kuliko kuku.

Wanatunza nywele na sura kuliko usichana wao. Ni wakati ambao maendeleo yanaenda kasi kuliko uwezo wetu wa kufikiri. Kizazi hiki kinahitaji maombezi mtambuka.

Paula kazaliwa kipindi ambacho maendeleo ya utandawazi ni makubwa kuliko imani ya dini zote. Mtoto anavutiwa zaidi kujua matumizi ya simu na mitandao kuliko madrasa na ‘sande skuli’. Kipindi ambacho wanaijua sura ya Davido kuliko ya Kardinali Pengo. Mama yake Kajala ni staa. Amekua staa kabla ya usanii wa kuigiza. Baba yake ni staa wa muziki hata kabla ya kukutana na mama yake. Toto la mastaa ‘automatikale’ litakuwa staa nalo. Ndo Paula. Bahati mbaya sana tena sana. Mara nyingi Paula amekuwa akihusishwa na upuuzi upuuzi mitandaoni.

Kumbe ni mtoto mdogo bado anayehitaji kulindwa na jamii. Lakini jamii ikamgeuza.

Hapo ndipo wenye akili wakajua shuleni yatatokea yaliyotokea.

Kajala alitaka Paula aishi kama yeye. Mtoto wa shule tayari alikuwa na kurasa zake mitandaoni. Anajibishana na mashabiki na mastaa kibao.

Elimu na huo upumbavu ni maji na mafuta. Ilikuwa ngumu mno. Kilichotokea hakikuhitaji mtabiri kujua kuwa kingetokea. Wazazi na walezi hizi lawama zinawavaa kama ngozi. Hazibanduki.

Maendeleo yamefanya taarifa za Paula ziwe wazi kama vazi la kahaba.

Bahati mbaya hiki kizazi cha nyoka, wanamtwisha mtoto mzigo mzito kwa kumponda utadhani aliwaibia waume zao. Ambao hawakuchangia senti kwenye ada ndo wa kwanza kumponda. Ukisoma maneno ya watu juu yake huwezi kuamini kama anayeongelewa ni mtoto wa miaka chini ya 18.

Tuwaonye mastaa wa kike kuepusha malezi na maisha yao ya mitandaoni. Pia ni ujinga kupeana moyo kwamba hata Bill Gates aliacha shule na kafanikiwa kimaisha. Bill Gates aliacha akiwa chuoni Havard, akili nyingi mpaka kuwazidi wahadhiri wake. Hakuacha akiwa kidato cha nne Mikocheni huko. Dunia hii elimu ndiyo kila kitu.

Ni mtoto anayehitaji faraja na muongozo badala ya kusutwa. Kawaida ni vicheche tu vikiwa utupu vyumbani mwao baada ya kudanga usiku kucha.

Ndo vinaongoza kuchamba watu mitandaoni. Uliza kama vinalijua hata jina la Waziri Mkuu. Hawajui zaidi ya kuchamba mitandaoni. Mpeni ‘breki’ Paula wa Kajala.