Simu za Huawei kukosa apps za Facebook, Messenger, WhatsApp, Instagram na Boomerang

Kutokana na Serikali ya Marekani kuwa na vikwazo na kampuni ya simu ya Huawei, wateja na watumiaji wa simu hizo watakosa app maarufu duniani za Facebook, WhatsApp na Instagram.

Wateja wa simu hizo watakosa Ap hizo baada ya Facebook ambayo inazimiliki kuitikia wito wa Serikali wa vikwazo dhidi ya kampuni ya simu za Huawei.

Facebook wameipa notisi Huawei kuwa simu zozote zinazotoka hivi sasa kwenye viwanda vya kampuni ya Huawei kutokuwa na apps zake za aina yoyote.

Apps zinazomilikiwa na Facebook Inc ni Facebook, Messenger, WhatsApp, Instagram na Boomerang.

Facebook imeungana na kampuni ya Google kuunga mkono katazo lililotolewa na Serikali ya Marekani dhidi ya kampuni za Huawei ikiwa ni pamoja na kukataza kampuni kufanya nazo biashara na wananchi wake kwa ujumla.

Ingawa simu zilizopo sokoni ambazo zina apps, zinafanya kazi kama kawaida.