Usajili wa nyota 11 ghali duniani (Mwaka 2016)

Hulk

Muktasari:

Dirisha la uhamisho na usajili wa wachezaji limekuwa wazi tangu Julai Mosi na litafungwa Agosti 31, tayari limeshuhudia klabu zikivunja benki na kunasa saini za baadhi ya wachezaji wa bei mbaya.

Hadi sasa wapo wachezaji 10 waliojiandikia rekodi ya kipekee ya kusajiliwa kwa bei ya juu. Ni nani wanaoingia kwenye orodha hiyo?

1-Hulk - Zenit kwenda  Shanghai SIPG  kwa Pauni 46.1 milioni

Baada ya misimu minne akiwa Ligi Kuu ya Russia akiichezea klabu ya Zenit St Petersburg, Mbrazili Givanildo Vieira de Sousa, maarufu Hulk hadi sasa ndiye mchezaji ghali zaidi aliyetua Ligi Kuu ya China  kwa Pauni 46.1 milioni.

2-Sadio Mane - Southampton - Liverpool – Pauni 36 milioni

Raia huyo wa Senegal amekuwa mchezaji mwenye asili ya Afrika aliyesajiliwa kwa kitita kikubwa, Pauni 36 milioni  akitokea klabu ya Southampton na kutua Liverpool ambako amefuata nyayo za watangulizi wake, Adam Lallana, Dejan Lovren na Nathaniel Clyne wote kutoka klabu hiyo ya  Saint Mary’s.

3-Granit Xhaka - Borussia Monchengladbach - Arsenal -Pauni 34 milioni

Xhaka ni usajili wa kwanza Arsenal msimu huu ambako kocha Arsene Wenger  ameimarisha kiungo. Raia huyo wa Uswisi aling’ara kwenye fainali za Euro 2016.

4-Michy Batshuayi - Marseille - Chelsea – Pauni 33.2 milioni

Klabu mbalimbali za Ligi Kuu England zilimtaka raia huyo wa Ubelgiji, lakini kocha Antonio Conte amemnasa kwa  Pauni 33.2 milioni.

5-N’Golo Kante - Leicester - Chelsea – Pauni 30 milioni

Baada ya kung’ara akiwa Leicester City na baadaye Ufaransa kwenye Euro 2016, kiungo huyo Mfaransa ametua Chelsea kwa Pauni 30 milioni.

6-Mats Hummels - Dortmund - Bayern – Pauni 31.5m

Beki wa kati wa Ujerumani amekuwa mmoja wa nyota wa Borussia Dortmund kutua  Bayern ambao ameungana na wenzake, Robert Lewandowksi na Mario Gotze kwa ada ya Pauni 31.5 milioni.

7-Eric Bailly - Villarreal – Man  United – Pauni 30 milioni

Bailly ambaye ni raia wa Ivory Coast ni Mwafrika mwingine kusajiliwa kwa bei mbaya baada ya kuwa usajili wa kwanza wa Jose Mourinho akiwa Manchester United  kwa Pauni 30 milioni akitokea Villarreal, Hispania.

8- Renato Sanches - Benfica - Bayern – Pauni 27.5 milioni

Bayern Munich ilimsajili kinda huyo wa miaka 18 bila kujua kuwa atakuwa shujaa wa nchi yake, Ureno kwenye fainali za Ulaya, Euro 2016 ambako akichangia kutwaa ubingwa. Alisajiliwa kwa Pauni 27.5 milioni kutoka Benfica.

9- Henrikh Mkhitaryan - Dortmund – Man United – Pauni 26.3 milioni

Baada ya rekodi yake ya mabao 11 na kupika mengine 15 kwenye mechi 31 za Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga akiwa Borussia Dortmund  msimu uliopita, raia huyo wa Armenia ametua Manchester United kwa kitita cha Pauni 26.3 milioni.

10- Miralem Pjanic – AS Roma - Juventus –Pauni 25.4 milioni

Baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Italia, Serie A kwa msimu wa tano, Juventus ilimsajili Pjanic raia wa Bosnia kwa Pauni  25.4 milioni akitokea AS Roma.

11-Grzegorz Krychowiak - Sevilla -PSG – Pauni 21.8 milioni

Krychowiak  alihusishwa na kuhamia Arsenal  kwa sababu kadhaa zikiwamo mafanikio yake akiwa Sevilla,  lakini wababe hao wa Ufaransa, Paris Saint-Germain waliwahi na kunasa saini yake. 