Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TUONGEE KIUME: Oa kwa huruma, tukuhurumie

Ukisoma kozi za utengenezaji wa filamu, moja ya misemo ambayo utaisikia mara kwa mara ni ‘producer na director’ ni kama mke na mume, uhusiano wao ni kama ndoa kabisa. ‘Director’ au kwa Kiswahili tunaita muongozaji ni mtu mwenye jukumu la usimamizi mkuu wa nyanja zote za kisanii kwenye filamu, yeye ndiye anayebeba maono ya filamu itakuwaje kuanzia namna ya picha zitakavyokuwa, taa zitakazotumika, sauti, waigizaji watakavyovaa na kuigiza na kadhalika.

Wakati mwenzake, ‘producer’ au kwa Kiswahili mzalishaji, kazi yake ni kuhakikisha maono ya muongozaji yanafanikiwa kwa asilimia 100 na hufanya hivi kwa kusimamia nyanja nyingine, hasa za kifedha; vitu kama bajeti ya filamu, malipo ya wasanii, huduma kama vyakula.

Na hata baada ya filamu kukamilika, hufuatilia vitu kama jinsi filamu hiyo itakavyofanyiwa matangazo na mauzo na jinsi pesa iliyotumika kuitengeneza itakavyorudi.

Kwa hiyo wakati ukisikia huo msemo wa ‘producer’ na ‘director’ ni kama mke na mume, utasikia na ushauri kwamba unatakiwa umchague ‘producer’ kwa umakini sana.

Jamani usichague ‘producer’ kwa sababu ni rafiki yako, kwa kuwa unampenda tu, kwa sababu hajapata kazi muda mrefu na usichague kwa kumuonea huruma.

Ndivyo vivyo hivyo kwenye kuoa. Mwanamume usichague mwanamke wa kuoa kwa huruma hata siku moja. Tumeshuhudia rafiki zetu wengi wakisema namuoa fulani kwa sababu ana ujauzito wangu, nyumbani kwao watamnyanyasa sana kwa kupata mimba nje ya ndoa nisipomuoa. Hongera kwa kutokuwa mbinafsi, kwa kuwawaza wengine, hilo ni jambo zuri, lakini kuoa kwa sababu ya kumuonea huruma tu, hiyo sio njia sahihi.

Hata sio marafiki zetu tu, sisi wenyewe, baadhi yetu tumeoa kwa sababu ambazo hazihusiani kabisa na ndoa, mtu anaamua kumuoa mtu kwa kuwa mwanamke alimsaidia sana kifedha kipindi alipokuwa hana kazi. Unafeli.

Kuna stori ilikuwa inazunguka mtandaoni, ya mwanamume ambaye alimchangia figo mwanamke, na mwanamke alipopona tu, akapata mchumba na kuolewa.

Watu wakawa wanasema kwamba mwanamke huyo ni katili. Kivipi? Hutakiwi kuolewa kwa sababu zisizohusiana na ndoa. Figo yako ni muhimu sana, imeokoa maisha yangu, lakini ndoa ina vitu vingi vya kuzingatia kuliko figo na ndiyo hivyo mtu anatakiwa avitazame kabla ya kuoa kwa sababu huwezi kuwa unanichangia figo kila siku tukishakuwa kwenye ndoa.

Oa kwa sababu huyu ndiye mtu unayetaka kuishi naye milele daima, oa mtu unayeamini anakupa furaha na anayeweza kuvumilia upungufu wake.

Itapendeza zaidi ukipata mtu wa aina hiyo ambaye pia anaweza kukusaidia kifedha ukiwa huna kazi, au anayeweza kukuchangia figo ukilazwa Muhimbili.

Yaani sababu nyingine zote zinatakiwa kufuata baada ya kuhakikisha sababu ya kwanza ipo.