Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasemavyo wasanii kuhusiana na kifo cha Ngwea

Muktasari:

  • Ngwea kapambana na muziki ukiwa hauna mbele wala nyuma kapambana kuhakikisha unakuwa bora lakini kwa sasa ndiyo unatambulika baada ya kufanya jitihada za kila aina kuufanya uwe ulivyo

Kutokana na kifo cha msanii Albert Mangwea ambaye amefariki nchini Afrika ya Kusini ambako alikwenda kufanya maonyesho, wasanii mbalimbali  wamezungumzia kifo chake.

Ni dhahiri, Albert Mangwea alikuwa katika kuutangaza muziki wa Tanzania nje ya nchi na ndiyo uhai wake ulikopotea, Mwandishi wetu Kalunde Jamal aliongea na baadhi ya wasanii wenzake na maongezi yakawa kama ifuatavyo:

Joseph Haule a.k.a Profesa Jay

Anasema katika hili hakuna jinsi kwa kuwa kila binadamu atayaonja mauti.

“Inaniuma sana lakini sina cha kufanya kwa kuwa ni kazi ya Mungu na kazi yake haina makosa, kinachotakiwa ni kumuombea apumzike kwa amani  huko aendako.         

Selamani Msindi ‘Afande Sele’

Anasema anamtambua Ngwea siyo kama msanii bali ni mdogo wake wa karibu na ameshindwa kujizuia kutoa machozi kuhusiana na kifo hicho.

Anaongeza kuwa katika kuonyesha ni kwa jinsi gani kijana huyo alikuwa na mapenzi na watu kwani kwao ni Morogoro lakini alijulikana ni kijana wa Dodoma almaarufu East Zoo.

Ngwea kapambana na muziki ukiwa hauna mbele wala nyuma kapambana kuhakikisha unakuwa bora lakini kwa sasa ndiyo unatambulika baada ya kufanya jitihada za kila aina kuufanya uwe ulivyo.”

“Sidhani kama atanitoka kichwani kwangu, naona kama ametutoroka kwa kuwa hatuhitaji aondoke muda huu lakini hakuna jinsi tutakutana naye siku ya mwisho na nitamweleza machungu yangu na kwa jinsi gani kifo chake kimeniumiza,” anasema.

Snura Mushi ‘Snura’

Anasema anasikitika sana hasa kwa wao ambao ndiyo kwanza wameingia kwenye muziki na walitaka kujifunza mengi kutoka kwa wasanii wanaofanya vizuri kama Mangwea, lakini kwa bahati mbaya au nzuri Mungu amechukua kiumbe chake hakuna cha kufanya kupinga hilo kwani haliwezekani.

Naseeb Abdul ‘Diamond’

Anasema ni juzi tu walikuwa Zanzibar katika mazishi ya mkongwe Bi Kidude kabla hawajasahu wanapoteza dhahabu nyingine kwenye tasnia hii ya muziki.

Anaendelea kuonyesha masikitiko yake kwa kusema kuwa mara ya mwisho kuwa naye ni siku waliokuwa wanafanya kazi ya Tundaman na waliongea mambo mengi ya utani ya kweli ya maisha wakicheka wakifurahi kumbe ndiyo ilikuwa safari yao ya mwisho kuwa pamoja kwa muda mrefu.

“Inauma lakini kuombeana ndiyo kinachotakiwa hakuna zaidi ya hapo kwa kuwa hakuna uwezo wa kupinga kazi ya Mungu ametuleta kwa makusudio maalumu na anatuchukua kwa makusudio pia na hatujui nani anafuata hivyo tuongeze upendo miongoni mwetu ili ikitokea mmoja wetu akafariki tumkumbuke kwa mazuri kama ilivyo kwa Ngwair,” anaasa Diamond.

Hadija Kopa

Anasema ukiachilia mbali kuwa alikuwa ni mwanamuziki mkubwa lakini yeye kama mzazi inamuuma sana kuona vijana wadogo ambao ndiyo wangekuja kubeba mikoba ya muziki wao watakapoondoka ndiyo wanatangulia mbele ya haki.

Anaonyesha majonzi yake zaidi kwa kusema kuwa kifo hakichagui na kusema sana ni kumkufuru Mungu, vijana wenzake wameuenzi kwa kuhakikisha hawatoki nje ya mstari hasa katika kuufikisha muziki unakotakiwa kufika.

“Amekufa akiwa katika kutafuta maisha yake kibaya zaidi ni kipindi ambacho vijana wengi wanajaribu kuuvusha nje ya mipaka muziki wetu na yeye ni moja ya vijana hao, nawaomba wasanii wachanga wafuate nyayoi zake kufanya hivyo ili muziki ufike mbali na usiishie Barani Afrika bali uende mbali zaidi”anasema Kopa.