Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CCM Songea yaanza mchakato kumpata mrithi wa Mhagama

Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama enzi za uhai wake.

Muktasari:

  • Mhagama ambaye alikuwa waziri katika Serikali za awamu tofauti, alifariki dunia Desemba 11, 2025, hivyo kuacha wazi nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

Songea. Ikiwa ni mwezi mmoja na siku sita tangu aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama afariki dunia, Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Songea kimetangaza mchakato wa ndani wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

Mhagama ambaye alikuwa waziri katika Serikali za awamu tofauti, alifariki dunia Desemba 11, 2025, hivyo kuacha wazi nafasi ya ubunge katika jimbo hilo.

Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini  Juma Nambaila

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa kwa umma na Katibu wa CCM Wilaya ya Songea, Juma Nambaila leo Januari 18, 2026, wanachama wenye sifa wametakiwa kujitokeza kutia nia ya kugombea nafasi hiyo ya ubunge.

Amesema uchukuaji na urejeshaji wa fomu utaanza leo Januari 18, 2026 na utafungwa siku inayofuata, Januari 19, 2026 na muda wa kuchukua fomu ni kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

Aidha, ametoa wito kwa wanachama wote wenye sifa na nia ya kugombea kuzingatia maelekezo ya CCM pamoja na kuhakikisha kuwa fomu zinarejeshwa ndani ya muda uliopangwa, huku zitakazorejeshwa nje ya muda hazitapokelewa.