Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kesi ya vigogo wa Chadema Dodoma yakwama kusikilizwa

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Stephen Karashan, (wa kwanza Kulia) akiwa kwenye kizimbani kwenye mahakama ya hakimu Mkazi Dodoma waliposomewa shtaka la kutishia kufanya fujo, katikati ni Katibu wa Chadema wilaya ya Dodoma mjini Azizi Abbas na kushoto ni  Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini Wiliam Keiya. Picha na Rachel Chibwete

Muktasari:

  • Vigogo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Dodoma Mjini hakusomewa hoja za awali kuhusu kesi inayowakabili ya kutishia kufanya fujo kama ilivyopangwa, kutokana na hakimu anayesikiliza kesi hiyo kutopkuwepo mahakamani.

Dodoma. Vigogo wa Chama cha Dmokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Dodoma Mjini leo wameshindwa kusomewa hoja za awali kuhusu kesi inayowakabili ya kutishia kufanya fujo, baada ya hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Zabibu Mpangule kutokuwepo mahakamani.

Washtakiwa hao ambao ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Stephen Karashani, Katibu wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Azizi Abbas na Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, William Keiya walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza, Juni 13, 2025 na kusomewa shtaka moja la kutishia kufanya fujo.

Washtakiwa wote watatu walisomewa shtaka hilo na kuhamasisha maandamano yasiyo na kibali, baada ya kukamilika mkutano wa hadhara uliofanywa na chama hicho Juni 8, 2025.

Kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikizwa hoja za awali leo, lakini Wakili wa Serikali, Daniel Lyatuu ameieleza mahakama mbele ya Hakimu Mkazi, Denis Mpelembwa kuwa hakimu anayesikiliza kesi hiyo hayupo, hivyo waliomba kupangiwa tarehe nyingine kwa ajili ya kusikiliza hoja hizo.

“Mheshimiwa washtakiwa wote watatu wapo mbele yako lakini hakimu anayesikiliza kesi hii, Zabibu Mpanguile amepata dharura za kiutendaji, yupo nje ya mahakama, hivyo tunaomba tupangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali,” amesema Lyatuu.

Upande wa utetezi ambao unawakilishwa na mawakili wa kujitegemea watano ambao ni Godwill Benda, Fred Kalonga, Meshack Ngamando, Deogratius Mahinyila na Josephat Mbeba walikubaliana na hoja hiyo ya kuahirisha kesi, lakini waliiomba Mahakama kuwapatia nakala ya maelezo ya mlalamikaji katika kesi hiyo.

Wakili wa Serikali, Lyatuu aliiambia Mahakama kuwa atawasiliana na upande wa pili ili kuyapata maelezo hayo na kisha atawakabidhi.

Baada ya maelezo hayo Hakimu Mpelembwa ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 15, 2025 ambapo washtakiwa hao watasomewa hoja za awali.

Washtakiwa wote watatu wataendelea kuwa nje kwa dhamana.