Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vigogo wa Chadema Dodoma wapandishwa kizimbani

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Stephen Karashan, (wa kwanza Kulia) akiwa kwenye kizimbani kwenye mahakama ya hakimu Mkazi Dodoma waliposomewa shtaka la kutishia kufanya fujo, katikati ni Katibu wa Chadema wilaya ya Dodoma mjini Azizi Abbas na kushoto ni  Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini Wiliam Keiya. Picha na Rachel Chibwete

Muktasari:

  • Viongozi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Dodoma Mjini wamepandishwa leo mahakamani na kusomewa mashtaka yanayowakabili na kisha kuachiwa kwa dhamana hadi Juni 27, 2025 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kusikiliza hoja za awali.

Dodoma. Viongozi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Dodoma Mjini wamefikishwa mahakamani leo na kusomewa shtaka moja la kutishia kufanya fujo.

Washtakiwa hao ambao wanawakilishwa na wakili wa kujitegemea, Fred Kalonga ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Stephen Karashan, Katibu wa Chadema Wilaya ya Dodoma mjini, Azizi Abbas na Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Dodoma Mjini, Wiliam Keiya.

Wote watatu wamesomewa shtaka hilo la kutishia kufanya fujo na kuhamasisha maandamano yasiyo na kibali baada ya kukamilikankwa mkutano wa hadhara wa chama hicho Juni 8, 2025 mbele ya hakimu Mkazi wa mahakama ya hakimu Mkazi Dodoma, Zabibu Mpangule.

Hata hivyo, washtakiwa wote watatu walikana mashtaka hayo ambapo walitakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja watakaosaini mali yenye thamani ya Sh5 milioni kila mmoja na wanatakiwa kuwa wakazi wa Dodoma.

Washtakiwa wote watatu walikamilisha masharti ya dhamana na waliachiwa huru kwa dhamana ambapo hakimu Mpangule aliwataka wadhamini hao kuhakikisha washtakiwa wanafika mahakamani kila siku ya kesi yao bila kukosa hadi itakapokwisha.

“Mkishindwa kuwasimmia washtakiwa kufika mahakamani kila siku ya kesi yao mali zenu mlizoandika kama dhamana zitauzwa na kama hazitakuwa na thamani ya Sh 5 milioni au zitaharibika mtafungwa kifungo cha miezi sita,” amesema Mpangule.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 27, 2025 itakapokuja kusikilizwa hoja za awali.