Mbowe amtaka Silinde aombe msamaha kwa usaliti

Muktasari:
- Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amehutubia wananchi katika mji wa Tunduma mkoani Songwe katika viwanja vya shule ya msingi Tunduma ambapo ameanza kwa kutamka Silinde na Fakii Lulandala kuwa ni wasaliti dhidi ya mageuzi.
Songwe. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amemtaka Naibu Waziri Tamisemi, David Silinde ambaye ni Mbunge wa Tunduma kumrejea Mungu kwa kuomba toba kutokana na dhambi ya usaliti aliyoifanya dhidi ya mageuzi.
Mbowe ambaye leo Ijumaa February 24, 2023 amehutubia wananchi katika mji wa Tunduma mkoani Songwe katika viwanja vya shule ya msingi Tunduma ambapo ameanza kwa kutamka Silinde na Fakii Lulandala kuwa ni wasaliti dhidi ya mageuzi.
“Kama Silinde ananisikia, aende kwenye kabila lake aombe msamaha kwa Mungu aliye na uwezo wa kusamehe, baada ya hapo anipigie simu nami nitamuelekeza nini cha kufanya na kiukweli Chadema tutamsamehe,” amesema Mbowe
Mbowe amesema amesikitishwa na kitendo cha jeshi la polisi kung’oa bendera za Chadema ambazo amesema hazina hatia yoyote pamoja na kuwaweka mahabusu wananchi wasiokuwa na hatia.