Mwenyekiti CCM Tabora arejea kwa kishindo

Hassan Wakasuvi (wa kwanza kushoto) ambaye ametetea nafasi yake ya uenyekiti. Wengine ni wagombea wenzake, Stella Masubo na Waziri Jumbe. Picha na Robert Kakwesi.

Muktasari:

Hassan Wakasuvi ametetea nafasi yake kwa kishindo ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tabora akipata asilimia 91.6 ya kura zote.

Tabora. Hassan Wakasuvi ametetea nafasi yake kwa kishindo ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tabora akipata asilimia 91.6 ya kura zote.


Ni katika uchaguzi uliofanyika leo Jumapili, Novemba 20, 2022 ambapo amewashinda wapinzani wake wawili ingawa mmoja alijiondoa.


Aliyejiondoa ni Waziri Jumbe ambaye hata hivyo alipata kura 14 na mpinzani wake Stela Masubo kupata kura 80 kati ya kura halali 1,124.


Msimamizi wa uchaguzi huo, Martin Shigela amesema Hassan Wakasuvi amepata kura 1,030 kati ya kura halali 1,124 sawa na asilimia 91.6 huku kura 5 zikiharibika kati ya kura 1,129 zilizopigwa.