Mwenyekiti Wazazi CCM aahidi kupandisha viwango

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Taifa, Fadhili Maganya akizungumza na jumuiya ya wazazi mkoani Arusha leo

Muktasari:

Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Fadhili Maganya amesema kuwa atahakikisha anaipandisha viwango jumuiya hiyo na kulinda kauli zake kwa matendo.

Arusha. Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Fadhili Maganya amesema kuwa atahakikisha anaipandisha viwango jumuiya hiyo na kulinda kauli zake kwa matendo.

Ameyasema hayo leo Novemba 28 wakati akikaribishwa rasmi na jumuiya hiyo jijini hapa.

Maganya amesema kuwa, atahakikisha anatumia makada wa chama hicho kuendeleza na kuinua mradi mbalimbali waliyo nayo.

Amefafanua kuwa, wataendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna yoyote ile.


Aidha ameitaka jumuiya hiyo kuleta miradi mbalimbali ili iweze kufanyiwa kazi kwani yeye anaamini katika uongozi unaoacha alama.

Maganya amefafanua kuwa, amejipanga kuhakikisha anajenga hospitali kubwa ya rufaa, benki, kiwanda cha nguo, pamoja na kuwa na mashamba ya mifugo ya kanda pamoja na miradi mingine mbalimbali.

Amewataka wana CCM kusahau matokeo ya uchaguzi na warejee kukijenga chama chao.

Kwa upande wake Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Musa Matoroka  amesema wana wajibu wa kutafuta kura katika uchaguzi wa  Serikali za Mitaa 2024 pamoja na uchaguzi mkuu wa ifikapo 2025.

Aidha ameitaka jumuiya hiyo kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kuhakikisha kura zinatosha na zinajaa.

Naye Mwenyekiti wa wazazi mkoa wa Arusha, Hezron Mbise amesema kuwa, jumuiya hiyo imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya ufugaji wa nyuki uliowaletea manufaa.