Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tumechanganywa na tumechanganyikana

Fyatu mwenzenu niliipata kinoma. Katika kupata ulabu si akatokea chawa mmoja akamshambulia rafiki yangu ambaye ni mchunaji, sorry mchungaji wa kujipachika. Ni wakati alipokuwa akisifia ufyatu wangu ninaotoa hapa. Fyatu sorry chawa alihamaki na kurusha matusi tena ya kitoto utadhani hakuwa fyatu mzima!

Nilipohoji kunani, alisema tena kwa kebehi ‘inakuwaje huyu unamruhusu achanganye dini na siasa?” Nilimuuliza anachanganya dini na na siasa vipi au wewe ndiyo unavichanganya wakati vyote viwili ni dugu moja? Fyatu chawa alijibu “nimewasikia mkilaumu kila kitu anachofanya maza. Halafu mnasifiana.” Bila kupoteza muda, nilimjibu kuwa kazi yetu siyo kumsifia yeyote awe maza au faza yetu. Kwani, yeye ni malaika asiyekosea?

Namshukuru huyu fyatu chawa maana, sikuwa na mpango wa kutumia wiki nzima nikifuatilia tulivyochanganywa, tukachanganyikiwa, kuchanganyana hadi kuchanganyika, kukachanganya uongo na ukweli vikachanganyikana kifyatufyatu. Hivi kuchanganya dini na siasa ni nini? Katiba wala sheria havisemi lolote! Je dini na siasa ni tofauti au watoto mapacha? Nitajibu swali hili mwenyewe, nawe uongezee. Kimsingi, taasisi hizi zina sifa zifuatazo:

Mosi, zote chimbuko lake ni ughaibuni kabla na wakati wa ukoloni. Umewahi kujiuliza kama kuna mchango wa wahanga kwenye kuanzishwa na kuingizwa vitu hivi ambayo hutumia maguvu yawe ya mitutu au imani? Sasa, jiulize na ujijibu mwenyewe.

Pili, vyote ni kolonishi, yaani, vinatawawala mafyatu na kuwatumia vitakavyo hata kuwachanganya kiasi cha kuchanganyikiwa na kuanza kuchukiana mbali na kunyonyana hata kunyotoana roho.

Tatu, vyote hutegemea mafyatu kama mashamba yao na kuvuna visipopanda. Vikipanda, hupanda maneno na kuvuna njuluku. Mfano, siasa hutumia ushawishi hata ahadi za uongo kuwaingiza mkenge mafyatu ilhali dini hutumia vitisho vya moto na ahadi za vinono kuwatwisha mkenge mafyatu. Hamjaona pale Ubunguo? Fyatu mwenye duka lake la kuuza roho kasepa. Mafyatu wanafanya nini? Si wanakutana kila j’pili na kupigwa na ndata wakitetea fyatu asiyeweza kujitetea? Kwanini wasimuachie god wake amtetee? Si aliwahi kujidai kuwa hatishwi na yeyote wala chochote? Atokee na kufyanya fyoko akione cha moto.

Tatu, vyote hutumia njuluku za mafyatu zwazwa bila kukaguliwa na yeyote kiasi cha kuwatajirisha matapeli wa kiroho na kuwasikinisha mafyatu zwazwa.

Nne, vyote hudai vimetoka kwa God. Utawasikia hata matapeli wa kujipachika wakisema wao ni mashushu au wawakilishi wa god. Wanasiasa wakiukwaa ukuu, watakwambia maulaji yote hutoka kwa god. Hivi maulaji ya nduli au M7 yametoka kwa God? Mbona hamjui kitu rahisi hivi!

Tano, vyote uahidi unono hata kama mwishowe ni uchungu. Kila siku, utasikia wanasiasa wakiahidi kuleta maendeleo yasiyofika! Ukichunguza ni maendeleo ya nani? Hili sijibu. Jibu mwenyewe.

Sita, vyote hufanya matanuzi na kukemea wafuasi wake kuyachukia. Utamsikia mwanasiasa fisadi akilaani ufisadi majukwaani wakati ni ufisadi huo huo mtaji wake. Tapeli wa kiroho atakwambia mbinguni wataingia maskini ilhali yeye ni mkwasi!

Saba, vyote hupenda madaraka na ujiko. Kila palipo na kamera au waandishi wa umbea, lazima wawili hawa wawepo. Japo wanene wa dini hawakutangaza dini zao kama biashara, siku hizi, hata runinga na radio vinatumika kuwaingiza mkenge mafyatu.

Nane, vyote vilichanganyika tangu kuanza kwake kule Uropa ambapo popu alikuwa kiongozi wa lisrikal mbali na ntume naye kuwa mkuu wa dola. Kwani, hamjui au hamsomi historia?

Ngoja nichimbe zaidi. Dini na siasa vinachanganyikana na ni mapacha ila inategemea unavichanganyaje na kwa maslahi ya nani. Mfano, muimbaji wa nyimbo za injili akiimba nyimbo za kusifia wanene siyo kuchanganya dini na siasa. Akiimba za kukosoa, hapa, anachanganya dini na siasa kiasi cha kutishia amani na utulivu vya walaji na wanene.

Siasa inachanganyikana na kila kitu.

Mosi, mfano, mjeshi akiteuliwa kwenye nafasi ya kisiasa hachanganyi ugeshi na siasa?

Pili, ndata akisimamia uchakachuaji au kupendelea chama twawala, hachanganyi undata na siasa? Nani anahoji au kukataza?

Tatu, mchungaji wa bandia akijiunga na watawala, hachanganyi dini na siasa. Ila akikengeuka kutaka kuendelea kuwatumia, anaambiwa achanganya dini na siasa!

Nne, waumini wakintetea bosi kwa sababu ni dini moja, wanachanganya siasa.

Na lazima waonywe hata kufungiwa kwa kuleta udini na kuchanganya dini na siasa.

Tano, wanasiasa wakiapishwa kwa vitabu vya dini, kuombe, ‘kubarikiwa’, kuchangia asasi za kidini, au kuhudhuria kusimikwa kwa viongozi wa kidini, hawachanganyi dini na siasa! Sita, waumini au viongozi wakilipa kodi wakahoji matumizi yake, wanachanganya dini na siasa!

Saba, dini zikiwahimiza waumini kushiriki uchaguzi na kuchagua chama twawala, hawachanganyi dini na siasa.

Mwisho, tunaposema dini na siasa havichanganyiki wakati tunavichanganya, huku si kufyatuka kuchanganyana na kuchanganyikiwa? Basi, tuchanganyeni tuchanganyikiwe tuchanganye na kuchanganyikiwa kama lengo ni kutenda haki na kuleta maendeleo ya kweli.