Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujerumani yamtia doa Trump

Muktasari:

Jarida la Der Sipeger la Ujerumani limenukuu taarifa iliyoandikwa na wizara hiyo ikisema Marekani itategemea kushuka kwa pato lake la ndani yaani GDP, viwango vya ajira na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira ikiwa  Trump atapewa nafasi ya kulitawala taifa hilo.

Berlin. Wizara ya Uchumi ya Ujerumani imesema uchumi wa Marekani utaporomoka  endapo mgombea wa urais wa Chama cha Republican, Donald Trump atashinda katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Novemba 8 mwaka huu.

Jarida la Der Sipeger la Ujerumani limenukuu taarifa iliyoandikwa na wizara hiyo ikisema Marekani itategemea kushuka kwa pato lake la ndani yaani GDP, viwango vya ajira na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira ikiwa  Trump atapewa nafasi ya kulitawala taifa hilo.

“Ikiwa Trump atashinda urais nchini Marekani uchumi wa nchi hiyo utaporomoka kwa kasi,’’ ilisema sehemu ya taarifa hiyo

Trump mwenyewe amekwisha kuahidi kuwa atashusha makato ya kodi kwa kiwango kikubwa katika historia ya Marekani akichaguliwa kuwa rais.

Kauli hiyo ya wizara ya Ujerumani inaongeza nyingine kama hizo zilizotolewa katika mfululizo wa ukosoaji dhidi ya Trump katika kipindi cha wiki iliyopita huku magazeti ya kihafidhina yakikataa kumuidhinisha mgombea huyo na hata wanasiasa wa Ujerumani kumshambulia moja kwa moja.

Mgombea huyo anachuana na mgombea wa Chama cha Democrat, Hillary Clinton katika kinyang’anyiro hicho.