Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: CCM yafurahia kuondolewa kwa zuio la mikutano ya hadhara

Katibu Mkuu wa Chama cha CCM, Daniel Chongolo akizungumza kwenye mkutano wa 10 wa uchaguzi wa Jumuiya ya Wanawake (CCM) ngazi ya Taifa (UWT) uliofanyika jijini Dodoma umatatu Novemba 28, 2022.

Muktasari:

  • Katibu Mkuu Chongolo amempongeza Rais Samia kwa uamuzi huo huku akiahidi kwamba watakwenda kufuata sheria, taratibu na miongozo iliyowekwa na Serikali katika kuongoza mikutano ya hadhara hapa nchini.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amesema chama hicho kimefurahishwa na uamuzi wa Rais Samia wa kuruhusu mikutano ya hadhara na kwamba watakwenda kutumia fursa hiyo kuelezea yale yaliyofanywa na Serikali.

Chongolo ameyasema hayo leo Jumanne Januari 10, 2023 huko Unguja, Zanzibar wakati wa kilele cha matembezi ya vijana kuadhimisha miaka 59 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar, Rais Samia akiwa mgeni rasmi wa sherehe hizo.

Januari 3, 2023, Rais Samia alitangaza kuondoa zuio la mikutano ya hadhara lililowekwa mwaka 2016 na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli huku akivitaka vyama vya siasa kuzingatia sheria, kanuni na utamaduni wa Watanzania.

CCM yafurahia kuondolewa kwa zuio la mikutano ya hadhara

Katibu Mkuu Chongolo amempongeza Rais Samia kwa uamuzi huo huku akiahidi kwamba watakwenda kufuata sheria, taratibu na miongozo iliyowekwa na Serikali katika kuongoza mikutano ya hadhara hapa nchini.

“Chama cha Mapinduzi kimefurahishwa sana na uamuzi wako wa kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa. Kwetu sisi, CCM, hiyo ni fursa muhimu na kubwa sana kwani tunakwenda sasa kuitumia kuelezea umma kile ambacho serikali zetu zinakifanya katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama chetu.

“Hiyo fursa wala usiwe na wasiwasi nayo, tupo vijana, tupo makamanda wako, tunakuhakikishia tutaitumia ipasavyo kupeleka kwa umma kile ambacho mnakifanya wewe na Rais Mwinyi wa Zanzibar,” amesema Chongolo.

Vilevile, Chongolo amempongeza Rais Samia kwa kuunda kikosi kazi kwa ajili ya kupitia mfumo wa haki jinai, hatua ambayo amesema ni utekelezaji wa ilani ya CCM ambayo imeahidi kuhakikisha haki inatendeka hapa nchini.

“Kwa niaba ya CCM tuko timamu kuhakikisha yale unayoyafanya yakiwemo yale uliyopewa kibali cha kuyatekeleza na mkutano mkuu wa CCM ya kufanya mabadiliko ili kuimarisha serikali unayoiongoza. Tutahakikisha tunakusemea pale panapohitaji kukusemea,” amesema Chongolo.