Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hili la ‘mashangazi’ dalili ya tatizo kubwa

Katika gazeti wiki zilizopita tumeandika kwa kirefu kushamiri kwa matatizo ya vijana hapa Tanzania kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wanaowazidi umri maarufu kama ‘mashangazi’.

Kwanza tunampongeza Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango kwa kulishikia bango tatizo hilo linaloangukia katika mmomonyoko wa maadili na tamaduni za Kitanzania, pia tunaunga mkono hoja ya kutaka kufanyika kwa utafiti na kutafuta suluhisho haraka.

Kama ambavyo Dk Mpango alionyesha kusikitishwa na kukemea mwenendo huo mpya wa mahusiano, tunakubaliana naye kuwa kundi la vijana wadogo wanaingia katika mahusiano hayo kama njia rahisi ya kupata ufadhili wa kujikimu kimaisha.

Dk Mpango alibainisha kuwa huo sio utamaduni mzuri na haupaswi kuendekezwa na hivyo kutoa rai ya kufanyika kwa utafiti wa kisayansi ili kujua kiini cha mmomonyoko huo wa maadili na njia za kukabiliana na hali hiyo.

Ni utamaduni ambao haujazoeleka na ni mgeni kwa kijana mwenye umri mdogo wa miaka 20 hadi 30 kuishi na mwanamke mwenye umri wa zaidi ya miaka 40 kwa sababu tu mwanamke huyo ndiye anamhudumia kijana huyo kwa kila kitu.

Baadhi ya vijana hawa wadogo kiumri muda mwingi wako kwenye klabu za mazoezi (Gym), kucheza kamari (betting) na kwenye maeneo ya starehe na wengi wao hawana mwamko wa kufanya kazi kwa kuwa wanapata kila kitu.

Hili si jambo la kufumbia macho kwa kuwa dalili ya tatizo kubwa zaidi kwenye jamii yetu. Kwa kuendekeza tabia hizo tutakuwa tunajenga kizazi cha vijana wavivu na wasiowajibika kwa kwao wenyewe na kwa familia zao hapo baadaye’

Tatizo halipo upande huo tu, hata wanaume watu wazima wamekuwa na mahusiano ya kingono na wasichana wadogo wakiwalaghai kwa fedha na vitu vingine vya thamani, suala ambalo pia linapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Ukiangalia ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikiangazia sensa ya watu na makazi 2022, idadi ya vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 35 Tanzania Bara, ambao ndio wanaoathirika zaidi milioni 20.6, kati yao wanaume ni 9.8 milioni.

Ni kweli kundi la vijana hivi sasa linakabiliwa na tatizo kubwa la ajira na inakadiriwa kati ya vijana milioni moja wanaokomaa na kuingia katika soko la ajira kila mwaka nchini, 200,000 wanaopa ajira.

Hao 800,000 hawana uhakika wa kipato na baadhi yao ndio huangukia kwa mashangazi na matukio mengine ya mabaya kimaadili.

Kama alivyosema Dk Mpango, kuna haja ya kufanya utafiti juu ya desturi na utamaduni huu mpya kwa vijana wasiopenda kazi, lakini utafiti huo utatwambiwa kama mashangazi ndio huwashawishi hao vijana au kinyume chake.

Katika nchi zilizoendelea ni jambo la kawaida kwa mzee wa miaka 50 au 60 kuoa msichana wa miaka 25 au kijana wa miaka 25 kuoa mwanamke wa umri wa miaka 50 kwa sababu ni utamaduni wao, kwa Tanzania ni jambo geni na halijazoeleka.

Ni lazima utafiti utuambie, je utamaduni wetu kama Watanzania umebadilika, je, ni kweli tatizo la ajira kwa vijana ndio limeibua utamaduni huu mpya, na ni lazima utuambie tunatokaje hapo kurudi katika tamaduni zetu.