Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwitikio wa VVU: Fursa katika teknolojia na usawa

Desemba Mosi kila mwaka, dunia huadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani. Siku hii inatoa fursa ya kusherehekea maendeleo yetu kwa miaka zaidi ya 40 iliyopita ili kutambua kazi iliyo mbele yetu, kubaini changamoto na mafanikio tuliyopata katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu.

Kwa hapa nchini, maambukizi ya virusi vya Ukimwi, bado ni changamoto kubwa. Kwa mujibu wa makadirio ya mwaka 2023 ya Programu ya Pamoja ya Umoja wa Mataifa kuhusu VVU na Ukimwi (UNAIDS), takribani asilimia 87 ya watu wanaoishi na VVU wanafahamu hali yao na asilimia 82 wanapata matibabu ya kudhibiti virusi (ART) na asilimia 79 wameweza kufikia kufubaza virusi.

Makadirio hayo yanaonyesha pia wagonjwa 50,000 wenye maambukizi mapya ya VVU kwa mwaka 2023 na asilimia kubwa ya maambukizi haya hutokea miongoni mwa wasichana na wanawake.

Hivyo, ingawa kumekuwa na maendeleo mazuri, bado kuna upungufu katika mwitikiio wa kitaifa wa kupambana na VVU unaohitaji uangalizi wa karibu na haraka, hasa iwapo tunataka kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030.

Licha ya maendeleo mengi katika kinga na matibabu, kupitishwa kwa mikakati kama vile H = H (Havionekani = Haviambukizi) na teknolojia za muda mrefu za kuzuia VVU bado kuna changamoto. H = H ni mafanikio ya kisayansi ya mwaka 2011 yanayothibitisha kupungua kwa kiwango cha virusi kilichofubazwa kwa mtu anayeishi na VVU na hivyo virusi haviwezi kupitishwa kwa njia ya ngono.

Haya ni mapinduzi. Inamaanisha watu wanaotumia dawa zao za VVU kwa usahihi na kwa uthabiti hawana hofu ya kuwaambukiza wengine. Mkakati huu unajulikana kama matibabu, kama kinga au H = H (Havionekani = Haviambukizi), hivyo tutakuwa tunaua ndege wawili kwa jiwe moja.

Njia hii inatia moyo na kuhamasisha waviu kufuata na kubakia kwenye utaratibu wa kudhibiti virusi.

Jambo hilo huboresha afya, hufanya watu waishi muda mrefu kama watu wasio na VVU. Wakati huo huo, huondoa hofu na unyanyapaa dhidi ya waviu kwa hofu ya kusambaza VVU.

Ingawa mtazamo wa H=H umekubalika kote duniani, lakini kwa mujibu wa mwongozo wa WHO uliotolewa Julai 2023, uhamasishaji na utekelezaji wa sera nchini umedorora.

Mipango na kampeni za afya nchini lazima ziweke kipaumbele katika kuelimisha watoa huduma za afya na umma kuhusu H=H ili kupunguza unyanyapaa.

Kuongezeka kwa programu za H=H kutaboresha afya na kutufikisha kwenye mstari wa mwisho na hatimaye kufikia lengo la UNAIDS la asilimia 95 la kufubaza virusi.

Vivyo hivyo, pete ya uke au kitaalamu ‘dapivirine’ ni afua nyingine ambayo Tanzania inapaswa kupanga ili kuongeza ukubwa. Vilevile, sindano za kinga za muda mrefu zinazotoa ulinzi wa hadi miezi sita kwa wakati mmoja na zinawakilisha maendeleo makubwa katika kuzuia VVU. Aina hizi mpya ya kuzuia maambukizi kabla ya hatari (PrEP), inatoa mbadala wa vidonge vya kinga kila siku vya PrEP, ambavyo wengi hupata changamoto kuzingatia mara kwa mara.

Licha ya matarajio mazuri ya mikakati na teknolojia hizi, bado kuna vikwazo kama vile kuchelewa kwa sayansi ya utekelezaji, kuchelewa kuidhinishwa kwa udhibiti wa teknolojia mpya, uhaba wa mafunzo ya mara kwa mara kwa watoa huduma za afya na ufahamu wa jamii usiotosheleza unazuia uanzishwaji na utekelezaji wa ufanisi wa mikakati na teknolojia hizi nchini Tanzania.

Kadhalika, maendeleo ya hivi karibuni kuhusu ‘lenacavir’ yameonesha ufanisi mkubwa katika majaribio ya matibabu na kinga.

Kwa wale ambao hapo awali walikuwa wameshindwa kutumia aina nyingine ya tiba, ilibainika kuwa na zaidi ya asilimia 99 ya ufanisi katika kuzuia maambukizi ya VVU kwa matumizi ya kila miezi sita.

Njia hii inaweza kuleta mabadiliko tunayoyahitaji ikiwa itatekelezwa kwa ufanisi. Kampuni ya dawa hii-‘Gilead Sciences’ imechagua Tanzania kama moja ya nchi zilizopewa kipaumbele kupokea ‘Lenacapavir’ inayotolewa na Gilead hadi matoleo zalishi yatakapopatikana.

Tanzania haiwezi kumudu kubaki nyuma katika mwitikio wake wa VVU. Utekelezaji wa kina, madhubuti wa H=H, pete ya uke ya dapivirine, CAB-LA, na Lenacapavir siyo maamuzi tu, ni hatua muhimu kuelekea kufikia kizazi kisicho na Ukimwi.

Wakati Tanzania ikijitahidi kufikia malengo yake kudhibiti Ukimwi ifikapo mwaka 2030, lazima itangulize ubunifu huu na kuendana na kanuni bora za kimataifa ili kulinda na kuinua jamii zilizo na zinazoathiriwa na VVU na Ukimwi.