Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndoa ni darasa jifunze ufundishe wengine pia

Tuanze na kisa cha wanandoa wawili marafiki na wageni waliotutembelea hapa nyumbani. Walitoka Toronto kuja Manitoba. Hivyo, ilibidi walale angalau tujadili hili na lile.

Baba anatoka nchi jirani ya Tanzania. Mama ni Mkanada mzaliwa wa Toronto. Ilipofika wakati wa kulala, tuliwakumbusha watoto wetu kwenda kupiga miswaki na kwenda vyumbani.

 Na sisi tuliwaaga wageni wetu kuwa tunaenda maliwatoni kupiga mswaki. Wale wanandoa walitushangaa kwa nini tunapiga mswaki kabla ya kulala.

Nasi tuliwashangaa kwa nini wanahoji. Mama alisema akipiga mswaki wakati anakwenda kulala, asingeweza kupata usingizi! Nesaa naye alimwambia kuwa akilala bila kupiga mswaki, asingepata usingizi mbali na kukosa usingizi.

 Hivyo, tulishangaana. Sasa unaweza kujiuliza. Kama una mazoea safi ya kupiga mswaki kila ulalapo, utajiuliza hata kushangaa inakuwaje walale bila kupiga miswaki. Ukiangalia kisa hiki, kinahusu jambo dogo lakini lenye umuhimu mkubwa na la binafsi, lakini kinaweza kukufunza mengi. Je, ni mangapi wanandoa hawayajui japo ni muhimu?

 Mnapofunga ndoa, kila mmoja anakuja na mambo yake, yawe mazuri au mabaya. Kila mmoja anakuja na mazoea yatokanayo na malezi, mazingira hata uchaguzi na utashi wake. Ni kapu mchanganyiko. Hivyo, mnapoanza kuishi kama wanandoa, jambo kubwa na la muhimu ni kuwa tayari kujifunza na kufundisha. Ndoa ni shule isiyokuwa na mwisho.

 Ili kuifanikisha, wanandoa bila kujali viwango vya elimu au umri, lazima wawe tayari kuwa wanafunzi na walimu kwa wakati mmoja. Ukiangalia hili la kutopiga mswaki wakati wa kulala, pia laweza kuwapo la kulala bila kuoga.

 Binadamu ni viumbe wachafu. Unapolala mchafu, unategemea kweli mambo yaende vizuri? Umeshinda unakula, kujisaidia, kutoa jasho na mengine. Sasa inakuwaje unalala mchafu?

 Je, kwa wale waliozoea kulala bila kupiga mswaki au kuoga hawajapata la kujifunza hapa? Je, wale wenye utamaduni wa kuyafanya haya hawana la kuwafundisha wasioyafanya?

 Binadamu tuna mazoea na mila tofauti na saa nyingine kinzani kiasi cha kuchekana na kuishia kujicheka bila kujua. Mfano, kuna jamii huko bara Asia ambayo huamini kulamba vidole ni kuonyesha kuwa chakula kilicholiwa ni kitamu!

 Ukila na kumaliza bila kulamba vidole wanakushangaa kama unavyowashangaa kwa kulamba vidole. Pia, huko huko, wapo wanaokula kwa kupwakia na wengine wakiongea.

Turejee kwenye ndoa kama darasa hata shule. Je, wewe au mwenzako alishawahi kukutana na mazoea, mila, au tabia ambazo ni tofauti hata kinzani na za mwenzako. Je, huwa mnafanya nini mnapojikuta kwenye hali kama hii? Kama hamjawahi, mkijikuta kwenye hali kama hii, mtafanya nini? Hapa hakuna jibu moja. La muhimu, ni wote wawili kuwa tayari kujifunza na kufundishana kuliko kila mmoja kushikilia lake ndiyo sahihi. Mfano, katika kisa cha kutopiga mswaki, kupiga mswaki wakati wa kulala ni bora kuliko kutofanya hivyo. Pia, katika kisa cha kupwakia kama wanyama na kuongea wakati wa kula, kukaa kimya ni bora kuliko kutofanya hivyo.

 Hata hivyo, tuonye. Mazoea ni magumu kuyaacha, hasa yanapokuwa sehemu ya makuzi na malezi ya binadamu.

 Tumalize kwa kushauri kuwa, katika kutatua matatizo kama hayo, wanandoa wanapaswa kuwa flexible (hatuna Kiswahili chake). Wawe tayari kujifunza na kufundisha na si mara moja, bali miaka yao yote.