Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sera makini za makazi zitawanusuru watu Dar

Muktasari:

Wakazi wa maeneo ya mabondeni ikiwamo Jangwani, bonde la mpunga na maeneo mengine wamekuwa mara kadhaa wakijikuta waathirika wa mafuriko wakati wa msimu wa mvua jijini Dar es Salaam.

Jiji la Dar es Salaam na maeneo yake limeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua ambazo zimekuwa zikinyesha kwa mfululizo tangu wiki iliyopita. Zaidi ya watu 10 wamepoteza maisha, miundombinu imeharibika na mali zimepotea.

Wakazi wa maeneo ya mabondeni ikiwamo Jangwani, bonde la mpunga na maeneo mengine wamekuwa mara kadhaa wakijikuta waathirika wa mafuriko wakati wa msimu wa mvua jijini Dar es Salaam.

Mbali na wakazi wanaokaa mabondeni, wakazi wengi pia wa jijini Dar es Salaam na majiji mengine hapa nchini hukutana na adha wakati wa mvua kutokana na miundombinu mibovu katika makazi yasiyokuwa rasmi.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinakabiliwa na changamoto ya huduma ya makazi duniani. kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Makazi Duniani UN-Habitat ya mwaka 2010, inakadiriwa kuwa asilimia 70 ya wakazi wa Dar es Salaam wanaishi katika makazi yasiyo rasmi. Pengine watu wamekuwa wakijiuliza hivi wakazi wa mabondeni kwa nini wasihame?

Pengine watu wanajiuliza Watanzania hawapendi maisha yao kwa kukiuka wito wa Serikali yao inayowataka kuhama katika maeneo hatarishi?

Kunaweza kukawa na majibu mengi kuhusu maswali hayo lakini majibu yake ni kwamba hatujawa na sera makini za kuwapatia maskini makazi bora.

Katika nchi nyingi duniani mifano ipo, maskini waliopo mijini hukaa karibu na mji. Mtu maskini siku zote anapaswa aishi mahali na hatumia gharama kubwa kwenda katika shughuli zake za kile siku.

Hatatumia fedha ya nauli kwenda hospitali ama kumpeleka mtoto shule. Hii ni kuwapunguzia makali ya maisha.

Kinachoshangaza zaidi ni kwamba programu zetu za kuboresha huduma ya makazi kama taifa zimekuwa hazijikiti katika kuwalenga wanyonge ambao ndiyo walipaswa kunufaika moja kwa moja.

Kwa mfano, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limekuwa na mtazamo usiokuwa na uhalisia wa kujikita katika kuwamilikisha watanzania nyumba kwa gharama nafuu ambayo inaanzia milioni 27 kwenda juu.

Taasisi za fedha, mifuko ya pensheni na kadhalika, ni vyombo ambavyo vinapaswa kurahisisha mchakato wa makazi kwa watu. Mtu asiyekuwa na uwezo, anahitaji sana uwepo wa miradi ya umma imsaidie hata kama hatomiliki nyumba lakini aweze kupata huduma ya makazi kwa bei nafuu.

Katika mataifa mengine, mashirika kama nyumba ya taifa ndiyo hutumika hata katika urahisishaji wa masuala ya mipango miji.

Mashirika ya makazi ya taifa huhusika kujenga majengo kwa ajili ya kutoa huduma ya makazi mijini.

Ifahamike kwamba Serikali ya Tanzania inapoteza mapato mengi kwa kuhalalisha biashara inayomruhusu wananchi kutoa huduma ya makazi kwa kuwapangisha wenzake bila kulipa kodi serikalini.

Jambo la kushangaza miradi ya NHC imekuwa ikilenga kuuza nyumba zake kwa gharama nafuu kuwapa fursa watu binafsi kununua na kutoa huduma hiyo ya makazi kwa kuwapangisha wenzao. Japokuwa kuna miradi inayolenga kupangisha wananchi, lakini msukumo uko katika miradi ya kumilikisha.

Kuamua kuwa na miradi ya kuuza badala ya kutoa makazi sio tiba ya changamoto zinazowakabili wakazi wa Dar es Salaam bali ni ukwepaji wa majukumu husika.

NHC inapaswa ijipime kutoa huduma ya makazi kwa Watanzania wenye kipato cha chini wasioweza kukopa na kujikita katika kumilikisha nyumba kwa wachache wenye uwezo.

[email protected] +255 717 492 023.