Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tuandae filamu zenye maadili mema

Kamera kazini

Muktasari:

Haikuwa hivyo kwa sababu, sanaa hizo mbili zilitekwa kwa kiasi kikubwa na mapokeo ya utamaduni wa nje, kiasi hata kile kidogo tulichojaribu kufanya kilikuwa na taswira ya kuiga ya wenzetu.

Miaka 20 iliyopita, inawezekana hakuna aliyekuwa kwenye nafasi ya kutabiri kwa usahihi kutokea kwa mabadiliko tunayoshuhudia sasa katika sanaa ya muziki na filamu.

Haikuwa hivyo kwa sababu, sanaa hizo mbili zilitekwa kwa kiasi kikubwa na mapokeo ya utamaduni wa nje, kiasi hata kile kidogo tulichojaribu kufanya kilikuwa na taswira ya kuiga ya wenzetu.

Jamii yetu ilikuwa mtumwa wa muziki wa nje, sanaa ya filamu nayo ilitekwa na picha Ulaya, Marekani na Asia.

Lakini leo hatuko tena huko. Tuna mambo ya kujivunia ambayo kwa kiasi kikubwa yanakidhi, maadili ya jamii ya Kitanzania, siyo kwenye muziki wala filamu. Hii ni hatua kubwa ya maendeleo.

Lakini wakati wasanii hawa wanaibuka kila kukicha, iko haja ya kuangalia mambo kadhaa ambayo yanaweza kuwa mwongozo mzuri wa kuimba kwa kufuata maadili ya Kitanzania.

Kwa maneno mengine, msanii ni lazima atofautishe mazuri na mabaya mbele ya jamii yake. Wasanii wanaoshindwa kuchuja mazuri na mabaya, basi ni rahisi kuipotosha jamini yake.

Msanii lazima awe upande wa jamii kupinga matendo mabaya, awe tayari kuiongoza jamii anapoona ipo sababu ya kufanya hivyo na siyo kukaa kimya wakati yeye ni alama na kioo cha kufunza na kuelimisha.

Leo hii tuna mifano mingi jinsi sanaa inavyoweza kuipotosha jamii bila kujali kama wahusika watafanya hivyo makusudi au bila kujua timizo la wajibu wa kuitumikia sanaa hiyo. Hivi sasa, sanaa ya filamu nchini ina mvuto wa wengi hasa ukizingatia imeendelea kupanua wigo wa umaarufu na mafanikio kila siku.

Ikumbukwe kuwa, matumizi mabaya ya fani hii yanaweza kuipotosha kabisa jamii, hivyo ipo sababu ya wahusika, kwa maana ya wasanii na watayarishaji kuwa makini ili kuepuka hali hiyo.

Filamu nyingi zimekosa sura ya kuishawishi jamii kujifunza au namna nyingine ya kuwa mwanga au kioo cha jamii. Sababu ni kwamba, nyingi zimejaa mambo ya kujifurahisha wahusika kuliko kufikisha ujumbe.

Jamii ya sasa iliyopanuka kimawazo kutokana na kukua kwa teknolojia katika kila sekta, haitegemei elimu ya mtu kupitia shule pekee, bali hata mazingira anayoishi. Mazingira anayoishi mtu yanatoa fursa nzuri ya kujifunza, kuelewa wajibu wake na hata kuelewa wajibu wa watu wengine na mahitaji ya jamii anayoishi kwa jumla.

Na hapa tunaweza kuichukua fani ya filamu kama sehemu ya kuelimisha jamii kupitia maudhui mazuri kutoka kwa wahusika. Tofauti ni kwamba, tunachokiona kwa wasanii wetu ni mambo ya kushangaza.

Udhaifu na uvivu wa ubunifu kwa wasanii wengi nchini, umelazimisha jamii kutopata ujumbe wa kweli kutoka kwenye fani hiyo na kujikuta ikienda njia tofauti. Kwa kuiheshimu fani ya filamu na wasanii wake, tunapenda kuwakumbusha kuwa makini katika utunzi na utengenezaji wa filamu zao kwa kuepuka mambo yasiyostahili mbele ya jamii.

Tungependa kuona wasanii wanatengeneza filamu zenye mrengo na mahitaji ya Kitanzania, kwani maadili mema ndiyo urithi tulioachiwa na mababu zetu tangu enzi hizo. Hatuna sababu ya kuiga mambo yasiyostahili ya kuidhalilisha Tanzania kupitia sanaa ya filamu.

Tuandae mambo ya kwetu kwa kuenzi utamaduni wetu wa miaka mingine. Mwisho ni vyema basi wasanii wetu wakatambua kuwa, wao ni kioo cha jamii na kwa sababu hiyo wana wajibu wa kuhakikisha sanaa inakwenda mbali zaidi katika kuelimisha na isiishie kwenye burudani peke yake.