Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Athari kuwatesa mabondia wengi

Dar es Salaam. “Ukiendekeza kucheza mfululizo utakuja kukosa stamina mbeleni, imewahi kunitokea kwenye moja ya mapambano yangu ambalo nilipigwa KO (Knock Out) mbaya,” anasimulia Francis Cheka, bingwa wa zamani wa dunia wa WBF.

Mbali na Cheka, bondia namba moja kwenye uzani wa super middle nchini, Twaha ‘Kiduku’ Kassim anasema kucheza mfululizo inategemea na matokeo yako ya pambano lililopita.

“Kama umepigwa KO, halafu hujajua afya yako kwa ujumla ikoje, kisha ukapigana tena, ukapigwa, hii hata kabla ya ushauri wa dakatrai si nzuri kiafya,” anasema Kiduku.

Akimtolea mfano nguli wa zamani wa Dunia wa uzani wa juu, Mike ‘Iron’ Tyson ambaye alimudu kucheza mapambano hadi matatu kwa mwezi, Kiduku anasema bondia huyo alipigana hivyo kutokana na aina ya matokeo aliyokuwa akipata.

“Tyson kama pambano ni la raundi 10, basi yeye hapigani raundi zote, atamaliza pambano kwa KO mapema raundi ya kwanza au ya pili, hivyo hatumii nguvu kubwa na hata kucheza mfululizo sio shida,” anasema.

Rekodi ya mapambano matatu mfululizo kwa mwezi, Tyson aliiweka Novemba, 1985 alipocheza Novemba Mosi, 13 na 22, moja alishinda kwa KO raundi ya kwanza na mawili kwa Technical Knock Out (TKO) raundi ya kwanza na ya pili, mapambano yote yalikuwa ya raundi nane.

Kuanzia 1997 hadi anastaafu, bondia huyo alicheza kila baada ya miezi mitatu na zaidi, huku mapambano yake ya 2000 hadi 2005 anastaafu akipishana zaidi ya miezi minane hadi mwaka kati ya pambano moja na jingine, matatu alipigwa KO, mawili alishinda na sare moja.

Mapambano hayo ni kuanzia lile la Andrew Golota la Oktoba 20, 2000 kisha akacheza na Brian Nielsen Oktoba 13, 2001 baadae Lennox Lewis, Clifford Etienne, Danny Willaims na Kevin McBride ndiye alimstaafisha kwa kipigo cha RTD.

“Ukimuangalia Tyson, mpangilio wa mapambano yake utaona alicheza mfululizo kwa kuwa hakutumia nguvu kubwa kwenye mapambano yaliyotangulia yote alishinda tena kwa KO, yale ambayo alipigwa baadae yalipishana kwa miezi mitatu na zaidi “ anasema Kiduku.

Anasema unapocheza mfululizo, ukamaliza raundi zote hata kama hukupigwa, kuna stamina unakosa, achilia mbali aliyepigwa kwa KO.

“Huyu akicheza mfululizo, anajitakia matatizo mengine, unapokuwa ulingoni unatumia nguvu kubwa, lakini pia afya yako ni kitu cha kuzingatia, umepigwa, hujafanya uchunguzi kujua madhara yake, unarudi tena ulingoni, unautengenezea matatizo mengine mwili wako,” anasema.

Cheka anasema kucheza mfululizo mfululizo kuna faida na hasara zake, ikiwamo bondia kuchoka na kukosa stamina, jambo ambalo lilimkuta yeye.

“Siku 20 kabla ya kushinda ubingwa wa Dunia kwa kumpiga Phiri Williams kwa pointi, nilitoka kucheza na Chiotcha Chimwemwe (pia alishinda kwa pointi), pambano la awali ni kama lilinijenga kucheza na Phiri, ila baadaye nilitetereka na kuna pambano nilipigwa kwa kukosa stamina,” anasema.

Miongoni mwa ‘wahanga’ wa kucheza mfululizo ni Karim Mandonga, ambaye alipochapwa na Shaban Kaoneka Julai 31, alipumzika siku 21 na kurudi tena ulingoni Agosti 22, 2022, ingawa safari hiyo alishinda.

Pambano jingine ambalo Mandonga angecheza mfululizo ni lile la Nassor Abdallah ambalo kama lisingefutwa lingepishana kwa siku 12 na lile la Daniel Wanyonyi ambalo alishinnda kwa TKO.