Kwa nini saa ya Pep Guardiola inauzwa Sh3 bilioni?
MANCHESTER, ENGLAND. JUMANNE wiki hii, Kocha wa Manchester City, Pep Guaridola, alivaa saa ngali zaidi duniani katika mchezo wa robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya walipotoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Real Madrid, ugenini kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Guardiola alivaa aina ya Calibre RM27-01, kutoka Kampuni ya Richard Mille yenye thamani ya Sh bilioni 3.5.
Toleo la saa hiyo, awali ilitengenezwa maalum kwa ajili ya nyota wa tenisi raia wa Hispania, Rafael Nadal, ikiwa na mchanganyiko wa madini mbalimbali ikiwemo titanium ya daraja la tano, alminiamu na lithiamu.
Duniani mpaka sasa, zipo 50 pekee, huku Guardiola ambaye ni mmoja wa makocha wa soka wanaolipwa zaidi duniani, ni mmoja wa wamiliki wachache wanaojulikana, hata baadhi ya mastaa matajiri duniani hawana kwani haipatikani kwa kila mtu. Kando na muonekano wake wa kuvutia. Saa hiyo aliyoivaa Guardiola, ni nyepesi zaidi duniani ikiwa na uzito wa gramu 18.83.
Kama chapa inavyoonesha, hiyo inajumuisha kamba na inafanikisha hili kwa kutumia nyenzo kama vile titanium ya daraja la tano, alumini na lithiamu kuunganisha pamoja Richard Mille 27-01.
HAIVUNJIKI
Richard Mille 27-01, ni kazi bora katika utengenezaji wa saa, kwani waundaji wake wanadai saa hiyo ni imara kiasi kwamba, haiwezi kuvunjika. Muundo wake ni maridadi na kisasa zaidi, kulingana na nyaya za mvutano zilizounganishwa kwa uangalifu, mvaaji haimbani sana, wala haimfanyi kuona kero wakati wa kufanya kazi zake.
Saa hiyo awali iliuzwa Sh bilioni 2.2, lakini baada ya muda, bei yake imeendelea kuongezeka. Kitendo cha mastaa kama Nadal na Guardiola kuivaa, kinazidi kuifanya saa hiyo kuwa ya kipekee zaidi.
RICHARD MILLE INAGHARIMU KIASI GANI?
Kwa wastani, saa ya Richard Mille thamani yake ni takriban Sh 513,710,000. Hata hivyo, kuna zingine za bei ya chini ambapo ya kuanzia ni Sh 218,326,750 kwa chapa ya RM 016.
KWA NINI RICHARD MILLE NI GHALI SANA?
Moja ya vipengele vinavyofafanua zaidi vya saa za Richard Mille ni vifaa vinavyotumiwa katika kuitengeneza kwake. Saa hizi hazijatengenezwa kutoka kwa chuma cha kawaida au dhahabu. Badala yake, hujumuisha nyenzo za hali ya juu na ubunifu, na kuchangia lebo zao za bei ghali.
JE, IMEMGHARIMU KIASI GANI JAY Z KUWA NA SAA ZA RICHARD MILLE?
Inaelezwa kwamba, mkusanyiko wa saa za kifahari za Jay Z una thamani ya Sh bilioni 6.4, ambapo staa huyo alihitaji saa 3,000 aina za Richard Mille 56, ikielezwa ziligharimu kiasi hicho cha fedha.
NANI MMILIKI WA BRANDI YA RICHARD MILLE?
Richard Mille ni kampuni ya kifahari ya saa ikiwa imeanzishwa mwaka 2001 na Dominique Guenat akishirikiana na Richard Mille, inapatikana huko Les Breuleux nchini Switzerland.
....
SAA GHALI ZAIDI DUNIANI
Ukiachana na saa za Richard Mille ambazo ni ghali zaidi duniani, kuna saa zingine nazo zinashikilia rekodi ya kuwa za bei mbaya ambazo ni;
Graff Diamonds Hallucination – Sh 141,270,250,000
Graff Diamonds The Fascination – Sh 102,742,000,000
Breguet No. 160 – Sh 77,056,500,000
Chopard 201-Carat Watch – Sh 64,213,750,000
Patek Philippe Supercomplication – Sh 61,645,200,000
Jacob & Co. Billionaire Watch – Sh 46,233,900,000
Paul Newman’s Rolex Daytona – Sh 45,720,190,000
Patek Philippe Ref. 1518 – Sh 28,510,905,000
Vacheron Constantin 57260 – Sh 20,548,400,000
Hublot Big Bang – Sh 12,842,750,000