Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu tatu Metacha kurudi Yanga

Dar es Salaam. Mambo matatu yamechangia kurejea kwa kipa Metacha Mnata katika kikosi cha Yanga baada ya timu hiyo kuachana naye Juni 2019 kwa sababu za utovu wa nidhamu.

Kipa huyo aliyekuwa akiidakia Singida Big Stars ni mchezaji wa mwisho kutambulishwa kusajiliwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili lililofungwa juzi Jumapili, baada ya Mudathir Yahya, Kennedy Musonda na Mamadou Doumbia.

Majeraha ya kipa Abuutwalib Msheri ambaye amefanyiwa upasuaji wa goti, ni sababu kuu iliyochangia Yanga kuamua kumchukua Metacha kwa mkopo katika dirisha dogo la usajili.

Habari za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimefichua kuwa Msheri atakuwa nje kwa muda mrefu na hivyo kuiacha Yanga na makipa wawili tu ambao Djigui Diarra na Erick Johora huku wakikabiliwa na mechi nyingi ngumu za mashindano ya Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho la Azam na Kombe la Shirikisho Afrika.

Johora ameonekana kuachwa mbali kiubora na Diarra na tathmini ya haraka ambayo Yanga waliifanya, iliangukia kwa Metacha ambaye amekuwa chaguo la kwanza la Singida Big Stars na hudakia pia Taifa Stars.

Sababu ya pili ni kuepuka kutumia gharama kubwa kwani italazimika kumlipa mshahara tu tofauti na iwapo ingeamua kusajili kipa mwingine ambaye anaweza kuleta ushindani kwa Diarra ambapo ingelazimika kumnunua moja kwa moja kwenye timu yake kwa mahitaji ya muda mfupi tofauti na Metacha ambaye Singida Big Stars imekuwa rahisi kumuachia kutokana na mahusiano yao na Yanga.

Ukiondoa hizo mbili, uchache wa makipa walio kwenye kiwango bora kwa sasa ni sababu nyingine iliyopelekea Yanga kuamua kumsajili Metacha badala ya wengine.

Ukiondoa Diarra, makipa wengine ambao angalau wamekuwa wakionyesha muendelezo mzuri wa ubora msimu huu ni Aishi Manula, Hussein Abel na Metacha.

Isingewezekana kwa Yanga kumsajili Manula na pia Hussein Abel aliyekuwa akidakia Tanzania Prisons, amejiunga na KMC katika dirisha dogo la usajili hivyo aliyebakia alikuwa ni Metacha.

Kipa wa zamani wa Yanga, Peter Manyika alisema timu hiyo imefanya jambo sahihi kumnasa Metacha.

“Ni kipa mwenye uzoefu wa mechi za ndani na za kimataifa na amekuwa akifanya vizuri. Sina shaka na uwezo wake naamini atamsaidia vizuri Diarra,” alisema Manyika.

Kipa wa zamani wa Mtibwa Sugar, Said Mohammed ‘Nduda’ alisema Metacha ni kipa mzuri na ataisaidia Yanga.

“Anapenda ushindani na anakubali kujifunza pale anapofanya makosa. Naamini atakuwa na mchango kwa Yanga ukizingatia wana mechi nyingi ngumu mbele,” alisema Nduda.