Ajibu kuwakosa Simba

Friday December 31 2021
Ajibu1 PIC
By Charles Abel

Benchi la ufundi la Azam FC limesema kuwa kiungo mshambuliaji waliyemsajili jana kutokea Simba hatocheza katika mechi baina ya timu hizo kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ajibu amenaswa na Azam FC jana Desemba 30 kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Simba baada ya kuvunja mkataba wake wa miaka miwili aliokuwa nao awali.

Matumaini ya wengi yalikuwa ni kumuona Ajibu akicheza kesho lakini kocha wa Azam FC, Iddi Abubakar amesema kuwa kiungo huyo mshambuliaji hayupo katika mipango yao kesho dhidi ya Simba.

“Mpira ni kitu kinachoendana na mipango ya muda mrefu ambayo inaweza kubadilika kutokana na mahitaji ya mechi husika. Katika mchezo wa kesho ninaweza kusema kuwa kwa asilimia mia Ajibu hatokuwepo.

Ni mchezaji mzuri ambaye tunaamini ataisaidia timu lakini kwenye mechi ya kesho hayuko katika mipango,” alisema Abubakar.

Advertisement