Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal yaendeleza ubabe kwa Spurs, Moyes apigwa

Muktasari:

  • Arsenal imeshinda mechi nne kati ya tano ilizokutana na Tottenham hivi karibuni kwenye EPL

Arsenal imeendeleza ubabe dhidi ya Tottenham baada ya kuifunga mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliopigwa jana Januari 15, 2025 kwenye Uwanja wa Emirates.

Ushindi dhidi ya Tottenham unaifanya Arsenal kuonyesha ubabe kwani katika michezo mitano ya nyuma imepata ushindi mechi nne na kutoa sare moja.

Tottenham ilikuwa ya kwanza kupata bao ambalo lilifungwa na Heung-min Son dakika ya 25 kabla ya Dominic Solanke kuisawazishia Arsenal baada ya kujifunga kwa mpira uliopigwa kona dakika ya 40 baada ya kupigwa kichwa na Gabriel Magalhães.

Kabla ya kwenda mapumziko Arsenal iliandika bao la pili kupitia kwa Leandro Trossard dakika ya 44 ambaye alipiga shuti kali lililomshinda kipa wa Spurs Antonin Kinsky.  Mpaka dakika 90 zinamalizika Arsenal iliibuka na ushindi wa 2-1.

Matokeo haya yameifanya Arsenal ifikishe pointi 43 zikiwa ni nne nyuma ya vinara Liverpool na kukaa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya kucheza michezo 21.

Baada ya mchezo huo kocha wa Arsenal Mikel Arteta alisema: "Tunatafuta kwa nguvu na tutajaribu kufanya jambo kila mchezo ili tuone tunaweza kupata nini."

Bao alilofunga Heung-min Son linakuwa la nane dhidi ya Arsenal huku nyota wa zamani wa timu hiyo Harry Kane akiongoza kuifunga Arsenal akiwa na mabao 14.

Michezo mingine ya Ligi Kuu England iliyochezwa jana ilishuhudiwa Aston Villa ikichomoza na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Everton ukiwa ni mchezo wa kwanza wa kocha mkongwe zaidi kwenye Premier kwa sasa David Moyes.

Leicester City ikiwa nyumbani ilipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace na Wolverhampton ilifungwa mabao 3-0 ikiwa ugenini dhidi ya Newcastle.