Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz Ki ndani tena Burkina Faso

Muktasari:

  • Burkina Faso imeshafuzu fainali za Afcon 2023 baada ya kuongoza kundi B la mashindano hayo ya kufuzu kwa pointi zake 10 ilizokusanya katika mechi tano zilizopita.

Dar es Salaam. Kwa mara nyingine tena, nyota wa Yanga, Stephane Azizi Ki amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Burkina Faso kinachojiandaa na mchezo wa mwisho wa kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 dhidi ya Eswatini utakaochezwa Septemba 8 mwaka huu huko Marrakesh, Morocco.

Kiungo huyo pia alijumuishwa pia katika kikosi cha Burkina Faso kilichopoteza kwa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Cape Verde, Juni 18 mwaka huu katika mchezo wa raundi ya tano ya kufuzu fainali za Afcon.

Katika kikosi hicho kilichotangazwa leo na kocha Hubert Velud, Aziz Ki ni miongoni mwa nyota watano wanaocheza soka la kulipwa ndani ya bara la Afrika ambao wapo katika kundi la wachezaji 25 watakaoingia kambini mwanzoni mwa mwezi ujao kujiandaa na mechi hiyo wengine wakiwa ni Issoufou Dayo na Djibril Ouattara wa RS Berkane ya Morocco, Blati Toure wa Pyramids FC ya Misri pamoja na Valentin Nouma wa FC Lupopo ya DR Congo.

Beki wa Bayer Leverkusen ni miongoni mwa majina makubwa yaliyomo katika kikosi hicho cha Burkina Faso pamoja na mshambuliaji wa Bournemouth, Dango Ouattara na Issa Kabore wa Luton.

Licha ya kutokuwa na timu kwa sasa, kiungo Adama Guira amejumuishwa kikosini na kocha Velud lakini nahodha wa timu hiyo, Bertrand Traore anayeichezea Aston Villa hatyumo kundini

Kikosi hicho kinaundwa na makipa Herve Koffi (Charleoi), Kilian Nikiema (ADO Den Haag) na Sebastien Tou (Granolles) wakati mabeki ni Steeve Yago (Aris Limassol), Kabore (Luton), Dayo (Berkane), Adamo Nagalo (Norsdjaellund), Tapsoba (Leverkusen), Nasser Djiga (FC Basel), Abdoul Guiebre (Modena) na Nouma (Lupopo).

Viungo ni Dramane Salou (FC Urartu), Toure (Pyramids FC), Ismahila Ouedraogo (Panserraikos), Guira (hana timu), Sacha Banse (Standard Liege), Gustavo Sangare (Quevilly Rouen) na Aziz Ki (Yanga).

Wachezaji wa nafasi ya ushambuliaji ni Cyrille Bayala (Ajjacio), Mamady Bangre (Toulouse), Cedric Badolo (FC Sheriff), Abdoul Tapsoba (Amiens), Cheick Ouattara (Berkane), Mohamed Konate (Akhmat Grozny) na Dango Ouattara (Bournemouth).