Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bacca, Depu kuikosa TRA United, Pedro ashusha presha

Muktasari:

  • Yanga inaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 35.

Bundi wa majeraha ameendelea kulia ndani ya Yanga baada ya nyota wengine wawili Ibrahim Abdullah 'Bacca' na Laurindo Dilson 'Depu' kupata majeraha yatakayowafanya waukose mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kesho ugenini dhidi ya TRA United katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Taarifa ya Yanga imesema kuwa Bacca na Depu wamepata maejaraha tofauti ambayo yatawafanya wawe nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki mbili kila mmoja.

Wachezaji wengine ni Chadrack Boka na Edmund John.

"Ibrahim Abdullah (Bacca) amepata jeraha la nyonga na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha Wiki tatu. Laurindo Dilson (Depu) amepata majeraha ya nyama za paja na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili.

"Chadrack Boka amepata jeraha la enka ya mguu wa kushoto na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili. Edmund John amepata jeraha la Bega na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki mbili," imefafanua taarifa ya Yanga.

Wachezaji hao wameumia wakati tayari Dickson Job na Clement Mzize wakiendelea kuwa nje ya uwanja wakiuguza majeraha ya goti kila mmoja.

Pamoja na kuwakosa wachezaji hao, Kocha Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves amesema kuwa timu yake itajitahidi kuhakikisha inavuna pointi tatu keho.

"Tumekuwa na ratiba yenye msongamano mkubwa wa michezo ya mfululizo, na ukizingatia kuwa tumetoka katika mchezo mgumu wa ligi siku chache zilizopita, sasa tunajiandaa kuikabili timu ambayo imepata muda wa kutosha wa mapumziko na maandalizi.

"Hata hivyo, sisi ni timu kubwa yenye kikosi cha wachezaji bora wenye uwezo wa kukabiliana na mazingira ya namna hii," amesema Pedro.

Kocha huyo amesema kuwa anaamini mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Tabora United kesho utakuwa mgumu kutokana na kuimarika kwa wapinzani wao.

Kesho tunatarajiwa kukutana na timu ya TRA United, ambayo inaendelea kukua kwa kasi katika ligi yetu. Ni timu iliyoanzishwa hivi karibuni, lakini imeonesha maendeleo makubwa na ushindani wa hali ya juu.

Bila shaka, tunatambua kuwa hatutakuwa na mchezo mrahisi, lakini tuna imani kuwa itakuwa ni mechi nzuri kwetu"