Banda amaliza utata Simba, Yanga

Tuesday August 03 2021
bandapic
By Charity James

KLABU ya Big Bullets, imethibitisha kuachana na winga wao Peater Banda baada ya kufanya makubaliano na Simba ambayo imemsajili nyota huyo kwa mkataba wa miaka mitatu.

Muda mchache baada ya uthibitisho wa klabu yake ya zamani Simba wamemtambulisha winga huyo mpya kupitia mtandao wa kijamii Instagram.

Ujio wa Banda ndani ya Simba unathibitisha kuachwa Parfect Chikwende aliyesajiliwa na Simba akitokea FC Platnum ya Zimbabwe.

Banda ni mchezaji wa kwanza wa kigeni kusajiliwa na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajia kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika.

Advertisement