Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca yaibuka mtemi El Classico ikitwaa ubingwa La Liga

Wachezaji wa kikosi cha Barcelona wakishangilia taji la Ligi Kuu Hispania 'La Liga' walilotwaa baada ya kuwachapa mahasimu wao Real Madrid. Picha na Mtandao

Muktasari:

  • Taji la La Liga 2025/2026 ni la 29 kwa Barcelona ikizidiwa na Real Madrid ambayo inaongoza kwa kulitwaa ikifanya hivyo mara 37.

Barcelona, Hispania. Barcelona imetwaa kibabe ubingwa wa Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’ msimu huu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Madrid kwenye mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Nou Camp, Barcelona, Hispania.

Ushindi huo umeifanya Barca kufikisha idadi ya pointi 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote huku ligi hiyo msimu huu ikibakiza mizunguko miwili kufikia tamati.

Barcelona walionekana kutumia vyema udhaifu wa Real Madrid wa kuwakosa nyota wake muhimu kama Fede Valverde na Kylian Mbappe kuwafunga mabao hayo mawili yaliyowapa taji.

Wafungaji wa Barcelona katika mechi hiyo ni Marcus Rashford aliyepachika bao la kwanza katika dakika ya tisa na Ferran Torres ambaye amefunga katika dakika ya 18.

Hilo linakuwa taji la 29 la La Liga kwa Barcelona ambayo inaendelea kuwa timu inayoshika nafasi ya pili kwa kutwaa mara nyingi zaidi Kombe la Ligi Kuu Hispania.

Real Madrid bado inaendelea kuwa timu inayoongoza kwa kutwaa mara nyingi zaidi ubingwa wa La Liga ikifanya hivyo mara 36.


PSG ishindwe yenyewe


Nchini Ufaransa, PSG imejitengenezea mazingira mazuri ya kutetea taji la Ligi Kuu nchini humo ‘Ligue 1’ baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Brest.

Bao pekee la PSg katika mchezo huo limefungwa na Desire Doue katika dakika ya 81.

PSG sasa imefikisha pointi 73 ambazo ni sita zaidi ya zile za Lens iliyo katika nafasi ya pili.

Miamba hiyo ya Ufaransa inahitaji angalau matokeo ya sare katika mechi mbili ilizobakiza dhidi ya Paris FC na Lens.

Na hata kama ikipoteza na Lens ikashinda mechi mbili zilizobaki, PSG inaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kubebwa na utofauti mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa baina yake na Lens.

Wakati utofauti huo kwa PSG hivi sasa ukiwa ni mabao 44, Lens yenyewe utofauti wake ni mabao 29.