Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Beki Mtibwa afariki dunia, chanzo chatajwa

Beki wa Mtibwa Sugar (32), Iddy Mobby enzi za uhai wake.

Muktasari:

  • Aliyekuwa beki wa Mtibwa Sugar (32), Iddy Mobby amefariki dunia jioni ya leo Machi 5,2023 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.

Da es Salaam. Beki wa Mtibwa Sugar (32), Iddy Mobby amefariki dunia jioni ya leo Machi 5,2023 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.

Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru amethibithisha kifo cha mchezaji huyo kilichotokea leo ambapo alitaja chanzo cha kifo chake ni mshituko.

“Jana alipata mshituko kidogo, tukampeleka hospitali ya kiwanda cha Sukari Mtibwa hapa Manungu lakini wakatuelekeza tumpeleke Hospitali ya ‘Misheni’ tukampeleka kwa uchunguzi zaidi lakini nao wakatuambia anahitaji vipimo vikubwa.

Baada ya hapo ndipo tukampeleka Benjamin Dodoma na kufika saa 7 usiku, akapokelewa vizuri na vipimo mbali mbali vikaendelea na leo jioni ametutoka na sasa tunafanya taratibu za mazishi,” alisema Kifaru na kuongeza;

“Sasa naelekea Dodoma nikiwa kama mkuu wa msafara na baada ya hapo tutachukua mwili na kuelekea shinyanga kwaajili ya mazishi.”

Mobby alisajiliwa msimu huu wa 2022/23 akitokea Ruvu shooting ambapo jana Machi 4, mwaka huu mkoani Morogoro alipata tatizo hilo wakati akiwa katika mazoezi binafsi ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya KMC.

Beki huyo wakati wa uhai wake alizichezea timu mbalimbali za soka ikiwemo Geita Gold, Polisi Tanzania, Ruvu Shooting zote za Ligi Kuu katika nyakati tofauti pia alikuwa miongoni mwa mabeki wanaounda kikosi cha  timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’.