Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bingwa Carabao anachukua hela ndogo kuliko Ligi Kuu Bara

Muktasari:

  • Pesa hiyo ni ndogo ukilinganisha na mpunga ambao anapata bingwa wa Ligi Kuu Bara ambapo huchukua jumla ya milioni 600

London, England. Jana pale nchini England kulikuwa na mchezo wa fainali ya Carabao Cup kati ya Chelsea na Liverpool uliopigwa kwenye dimba la Wembley, mbali ya matokeo timu bingwa ilipata zawadi ya Pauni 100,000 ambazo ni sawa na milioni 322 za Tanzania.

Pesa hiyo ni ndogo ukilinganisha na mpunga ambao anapata bingwa wa Ligi Kuu Bara ambapo huchukua jumla ya milioni 600.
Mshindi wa pili wa michuano hii ya Carabao huweza kupata

Pauni 50,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 161 za Kibongo, wakati mshindi wapili wa Ligi Kuu Bara hukunja shilingi milioni 300.

Kwa upande wa timu zilizoishia hatua ya nusu fainali Fulham na Middlesbrough zenyewe zitapata Pauni 25,000 ambazo ni milioni 80, kwa pesa ya Tanzania.

Pesa hii ni kidogo sana ukilinganisha na kiasi ambacho anakipata bingwa wa Ligi Kuu England ambacho kinafikia Pauni 150 milioni na bingwa wa michuano ya FA Pauni 4 milioni.

Hata hivyo, michuano hii inaonekana kuzinufaisha zaidi timu za madaraja ya chini ambapo mapato yote yanayokadiriwa kufikia Pauni 80 milioni asilimia 45 hugaiwa kwa timu za kuanzia daraja la pili hadi la nne.

Pia ukiacha zawadi hizi timu hupata Pauni 100,000, ikiwa mechi yao hata moja itaonyeshwa kwenye televisheni.