Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fainali ya kikubwa Chelsea, Liverpool

Muktasari:

  • Baada ya kuvuka raundi tatu ngumu za mashindano hayo, timu hizo leo kila moja itakuwa na lengo la kurudi na Kombe nyumbani baada ya mechi hiyo ambayo kwa mujibu wa kanuni ikiwa itamalizika kwa sare katika dakika 90, zitaongezwa dakika 30 ambazo nazo zikimalizika kwa matokeo hayo, mikwaju ya penalti itatumika kuamua mshindi.

London, England. Chelsea na Liverpool zinaumana leo katika mchezo wa fainali ya Kombe la Calabao utakaochezwa katika Uwanja wa Wembley kuanzia saa 12:00 jioni kwa muda wa Afrika Mashariki.

Baada ya kuvuka raundi tatu ngumu za mashindano hayo, timu hizo leo kila moja itakuwa na lengo la kurudi na Kombe nyumbani baada ya mechi hiyo ambayo kwa mujibu wa kanuni ikiwa itamalizika kwa sare katika dakika 90, zitaongezwa dakika 30 ambazo nazo zikimalizika kwa matokeo hayo, mikwaju ya penalti itatumika kuamua mshindi.

Katika hatua ya nusu fainali, Chelsea iliitoa Middlesbrough kwa ushindi wa mabao 6-2 katika mechi mbili baina yao wakati Liverpool iliifunga Fulham mabao 3-2.


Liverpool hesabu tatu

Kwa Liverpool, ushindi wa mechi hiyo na kutwaa taji hilo vitakuwa na maana na thamani kubwa kwa sababu kubwa tatu, jambo ambalo hapana shaka litaifanya iipanie vilivyo mechi ya leo.

Sababu ya kwanza ni ya kuzidi kuboresha rekodi yao ya ubabe wa mashindano hayo ambapo hadi sasa miamba hiyo ya England inaongoza kwa kuchukua ubingwa wa Kombe la Calabao ikiwa imechukua ubingwa mara tisa ikifuatiwa na Manchester City iliyotwaa mara nane.

Kupoteza mechi yale maana yake kutaiwekea mazingira mazuri Man City kuifikia rekodi hiyo ya Liverpool na pengine kuipita ikiwa itafanya vizuri katika misimu inayofuata.

Lakini sababu ya pili ni Liverpool kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa mataji manne msimu huu ambayo ni hilo la Calabao, FA, Ligi Kuu na  Ligi ya Europa.

Na jambo la tatu ni kumpa uhakika Jurgen Kloop wa kuondoka na heshima klabuni hapo baada ya msimu kumalizika kufuatia uamuzi wa meneja huyo kutoendelea kuifundisha Liverpool katika msimu ujao.


Chelsea heshima

Mwenendo usioridhisha wa Chelsea katika Ligi Kuu ya England (EPL) unailazimisha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Kombe la Clabao leo vinginevyo mambo yanaweza kuwa mabaya kwa upande wao msimu.

Chelsea hadi sasa ina nafasi ya kutwaa mataji mawili tu ambayo ni Kombe la Calabao na lile la FA ambalo kwa sasa wapo katika raundi ya tano wakiwa wamepangwa kukutana na Leeds Unite.

Ikiwa nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi, Chelsea bado haina uhakika wa kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao na mashindano ya Europa hivyo kuchukua Kombe la Calabao kutaipa uhakika wa kumaliza msimu kwa heshima licha ya nyakati ngumu inazopitia.

Kama itafanikiwa kuchukua ubingwa leo, hilo litakuwa taji la sita la Calabao kwa Chelsea na hivyo kuifanya iikute Manchester United ambayo inashika nafasi ya tatu katika chati ya timu zilizochukua mara nyingi ubingwa wa Calabao ikifanya hivyo mara sita.

Chelsea pia inataka kumaliza ukame wa muda mrefu wa kutotwaa taji hilo ambapo mara ya mwisho ilichukua taji msimu wa 2014/2015.


Marefa hawa hapa

Refa wa kati katika mechi ya leo ni Chris Kavanagh ambaye atasaidiwa na Mark Scholes na James Mainwaring huku refa wa akiba akipangwa Tim Robinson ambaye atasaidiwa na Wade Smith.

Marefa watakaokuwa katika usimamizi wa teknolojia ya video ya usaidizi kwa marefa (VAR) ni John Brooks na Marc Perry.