Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Busquets astaafu na medali za dhahabu za mataji 27

Muktasari:

  • Busquets alijiunga na Inter Miam, Juni 23, 2023 akitokea Barcelona ambayo aliitumikia kwa zaidi ya miaka 15 kuanzia 2008 alipopandishwa kutokea kikosi cha vijana.

Kiungo wa Inter Milan, Sergio Busquets ametangaza rasmi kustaafu soka la ushindani jana Septemba 26.09.2025 huku akiondoka na kumbukumbu ya kushinda medali 27 za mashindano tofauti ya ngazi ya klabu na timu za taifa.

Kiungo huyu ameshinda mataji tisa ya Ligi Kuu Hispania 'La Liga', mataji saba ya Copa del Rey, mataji saba ya Supercopa de Espana na mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ameshinda mataji matatu ya UEFA Super Cup, mataji matatu ya Kombe la Dunia la Klabu, Ngao ya Mashabiki nchini Marekani na Kombe la Ligi Marekani.

Ametwaa mataji mawili akiwa na timu ya taifa ya Hispania ambayo ni Kombe la Dunia na Kombe la mataifa Ulaya.

Mbali na makombe hayo, Busquets amefanikiwa kuingia katika vikosi bora vya La Liha, Ligi Kuu Marekani, Kombe la Dunia, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Fainali za Euro.

Busquets alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Barcelona ambacho alikitumikia kwa miaka 15 kuanzia 2008 hadi 2023 katika michezo 722.

Ni wachezaji wawili tu ambao wamecheza idadi kubwa ya mechi ndani ya Barcelona kumzidi mabao ni Lionel Messi aliyecheza idadi ya mechi 778 na Xavi aliyecheza mechi 767.

Busquets amesema kuwa anaachana na soka akiwa hana anachoudai mchezo huo.

"Asanteni wote na asante sana mpira wa miguu. Siku zote utabakia sehemu ya stori hii ya kuvutia.

"Ninajihisi huu ni muda wa kusema kwaheri kwa kazi yangu kama mwanasoka wa kulipwa. Nimefurahia stori hii ya kipekee kwa takribani miaka 20, moja ambayo nilikuwa naota," amesema Busquets.