Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama akabidhiwa rasmi jezi yake Yanga

Muktasari:

  • Chama ambaye wengi walimzoea akiwa na jezi namba 17 Simba ambayo kwa upande wa Yanga ilikuwa ikivaliwa na Farid Mussa.

Dar es Salaam. Hatimaye kiungo mpya wa Yanga, Clatous Chama, amekabidhiwa jezi namba 17 ndani ya timu hiyo, ambayo wengi walizoea kumuona akiitumia wakati akiwa Simba.

Chama, mara baada ya kutua Yanga, alilazimika kutumia jezi namba 20 iliyokuwa ikivaliwa na Zawadi Mauya ambaye alitemwa.

Hata hivyo baada ya mazungumzo na winga Farid Mussa, aliyekuwa anaitumia jezi namba 17, amekubali kumpa Chama jezi hiyo.

Mapema Farid, alionyesha hana kinyongo kwa kumuachia Chama namba hiyo, endapo atahitaji kumuachia.

Kwa maamuzi hayo sasa Farid ambaye ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga, atakuwa anaitumia jezi namba 12 aliyochagua.

Kuonyesha maridhiano hayo Farid mwenyewe amemkabidhi Chama jezi hiyo wakiwa wameishika pamoja na kupeana mikono.

Akiwa Simba Chama kwa miaka mingi amekuwa akitumia jezi hiyo namba 17 ambapo hata alipoondoka na kurejea alirudishiwa na kuendelea kuitumia.

Kiungo huyo amejiunga na Yanga akitokea Simba kwa mkata wa mwaka mmoja baada ya kumaliza kandarasi yake Msimbazi.