Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama akubali yaishe Simba

Chama akubali yaishe Simba

Baada ya mijadala mingi mitandaoni kuhusu kiungo mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama 'Tripple C' kuongeza mkataba au lah kuitumikia timu hiyo hatimaye mambo yamewekwa hadharani.

Moja ya mjadala ambao ulishika kasi mitandaoni ni ule "kama amesaini mkataba mpya mbona picha hatuzioni?" ambapo ilikuwa kawaida wachezaji wakiongeza mkataba basi picha zao zingepostiwa kwenye akaunti za mitandao ya kijamii ya Simba SC.

Usiku wa kuamkia leo Januari 10, 2020 Mkuu wa Idara ya Habari wa klabu hiyo, Haji Manara ametuma picha kwenye mtandao wa wa Instagram zikimuonyesha Chama akisaini mkataba wa kuendelea kusalia klabuni hapo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji katika mkutano wake na waandishi wa habari mwaka jana alisema Chama ameongeza mkataba wa miaka mitatu.

Picha zilizosambaa jana mitandaoni ni wazi habari za kuondoka kwa Wekundu hao wa Msimbazi zitakuwa zimeisha na mashabiki watabaki na furaha.

Katika picha hizo Chama ameonekana akiwa na Dewji pamoja na Mtendaji Mkuu, Babara Gonzalez, Mshauri binafsi wa Dewji, Crescentius  Magori aliandika "Kuna maswali tuliulizwa mbona hakuna picha Clatous Chama  anasaini mkataba mpya Simba ?"

Chama kwasasa yupo mapumziko nchini kwao Zambia huku kikosi cha Simba kikiwa visiwani Zanzibar kwenye Mapinduzi Cup wakisubiri kucheza nusu fainali dhidi ya Namungo baada ya kuiondosha na kuivua ubingwa Mtibwa Sugar jana kwa mabao 2-0 ya ushindi.