Chama karudi huko! staa Simba afunguka

Friday January 14 2022
MKUDE PIC
By Mwanahiba Richard

Kiungo wa Simba Jonas Mkude amesema kuwa kurudi kwa Clatous Chama ni jambo jema ndani ya kikosi chao kwani ni mchezaji mzuri.

Chama ametambulishwa mchana wa leo kuwa mchezaji rasmi wa Simba baada ya kufikia makubaliano ya kimkataba na timu yake.

Mkude amesema kuwa ukiona uongozi unampigania mchezaji kumrudisha kikosi ujue kuwa mchezaji huyo ana umuhimu ndani ya timu.

"Chama ni mchezaji mzuri, kurudi kwake kunaonyesha kuna kitu anacho ambacho ataisaidia timu, hivyo arejee timu inamuhitaji katika kupambania mafanikio," amesema Mkude

Chama ambaye alikuwa anacheza soka la kulipwa nchini Morocco amerejea kwenye klabu yake ya zamani baada ya kufikia makubaliano ya kimkataba na timu yake ambayo hajamaliza hata msimu kuichezea.

Advertisement