Cheka ahamishia masumbwi Musoma

Bondia Francis Cheka

Muktasari:

  • Pambano hilo litakuwa la kwanza kwa Cheka kuzipiga katika mikoa ya kanda ya Ziwa.
  • Cheka alisema atakwenda kuzichapa Musoma na bondia kutoka katika nchi ya Zambia au Kenya.

Dar es Salaam. Bondia Francis Cheka amewakumbuka mashabiki wake wa kanda ya Ziwa baada ya kutangaza kucheza pambano lake la mwisho mjini Musoma.

Pambano hilo litakuwa la kwanza kwa Cheka kuzipiga katika mikoa ya kanda ya Ziwa.

Cheka alisema atakwenda kuzichapa Musoma na bondia kutoka katika nchi ya Zambia au Kenya.

"Bado tuko katika mazungumzo na mabondia wawili wa Kenya na Zambia, mmoja wapo natarajia kucheza naye pambano mjini Musoma.

"Nitacheza huko Juni kufuatia maombi ya mashabiki wangu  mbalimbali wa kanda ya Ziwa walionishauri nikacheze kule," alisema Cheka.

Kabla ya kwenda Musoma, Cheka atapigana na Daniel Wanyonyi kutoka Kenya pambano la kuhamasisha vijana kucheza ngumi litakalofanyika mjini Morogoro litakalofanyika Mei 6 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.