Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

City vs Chelsea mechi ya wakubwa Premier

Muktasari:

  • Man City inatakiwa kushinda mchezo huu ili kufufua matumaini ya kuwania ubingwa wa Premier.


London, England. Mashabiki wa soka, kesho watakuwa mbele ya televisheni zao kutazama mechi kali za Ligi Kuu England, lakini zaidi ni Man City dhidi ya Chelsea, saa 2:00 usiku.

Huu ni kati ya michezo ya ligi hiyo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa, kazi kubwa itakuwa kwa Man City ambayo inapambana kwa nguvu kubwa kuhakikisha inatwaa ubingwa wa ligi hiyo, lakini presha ipo kwa Chelsea ambayo haijafanya vizuri msimu huu.


Novemba mwaka jana, timu hizo zilimaliza mchezo wa mzunguko wa kwanza kwa sare ya mabao 2-2, yakiwa ni mabao mengi kuwahi kufungwa kwenye mchezo mmoja na timu hizo.
Chelsea yenye pointi 34 katika nafasi ya 10, inatakiwa kufanya kazi kubwa ya kumzuia staa wa Man City, Kevin De Bruyne ambaye amefanya vizuri kwenye timu hiyo kuanzia mwaka huu umeanza, akiwa ametoa pasi za mabao kwenye michezo minne mfululizo.

Kama De Bruyne atatoa pasi kwenye mchezo huu atakuwa mchezaji wa 11 kutoa pasi kwenye michezo mitano inayofuatana kwenye ligi hiyo.

Sasa ana pasi 66 za mabao tangu amejiunga na Man City, akiwa kwenye ligi hiyo amezidiwa na staa wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs  mwenye pasi 84.

City chini ya Pep Guardiola yenye pointi 52 ikiwa nafasi ya pili, imekuwa na kiwango bora msimu huu  inakwenda kwenye mchezo huu baada ya kushinda mechi 11 mfululizo kwenye mashindano yote.

Chelsea itacheza mechi hii ikiwa na nguvu baada ya kushinda michezo miwili iliyopita, dhidi ya Aston Villa (kwenye FA) na Crystal Palace kwenye Premier.

The Blues kwenye mechi hii itamtegemea zaidi Cole Palmer, ambaye amekuwa bora msimu huu akihusika kwenye mabao 16, amefunga 10 na kutoa pasi sita za mabao.

RATIBA
Leo, Jumamosi
Brentford vs Liverpool (Saa 9:30 alasiri)
Burnely vs Arsenal (Saa 12:00 jioni)
Fulham vs Aston Villa (Saa 12:00 jioni)
Newcastle vs Bournemouth (Saa 12:00 jioni)
Nottm Forest vs West Ham (Saa 12:00 jioni)
Tottenham vs Wolves (Saa 12:00 jioni)

Kesho, Jumapili
Sheffield Utd vs Brighton (Saa 11:00 jioni)
Luton Town vs Man United (Saa 1:30 jioni)

Keshokutwa, Jumatatu
Everton vs Crystal Palace (Saa 5:00 usiku)