Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dilunga mchezaji pekee Tanzania kucheza timu ya Afrika afariki, kuzikwa leo

Muktasari:

  • Mzee Dilunga anatarajia kuzikwa leo Alhamis saa 10.00 jioni, Kisarawe, mkoani Pwani huku akiwa ameacha wajane wanne na watoto 13.

Dar es Salaam. Mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya taifa 'Taifa Stars', Abbas Dilunga 'Sungura' amefariki dunia usiku wa kuamia leo Alhamisi nyumbani kwake Chanika, jijini Dar es Salaam.

Akiwa mchezaji wa timu ya Taifa' Mzee Dilunga aliwahi kuchaguliwa kuunda kikosi bora cha Afrika akiwa nchezaji pekee kutoka timu ya Taifa ya Tanzania, hii ni baada ya kucheza dakika chache akitokea benchi wakata timu yetu ya Taifa ikicheza na timu ya Taifa ya Nigeria, mjini Lagos.

Mzee Dilunga anatarajia kuzikwa leo Alhamis saa 10.00 jioni, Kisarawe, mkoani Pwani huku akiwa ameacha wajane wanne na watoto 13.

Dilunga ni baba mzazi wa mchezaji wa Ruvu Shooting, Said Dilunga baada ya kuacha soka miaka ya nyuma alianza kujihusisha na masuala ya uganga wa jadi ambapo shughuli zake alikuwa akizifanyia mtaa wa Jangwani.