Dube arejea Zimbabwe, asaini miaka miwili Hardrock
Muktasari:
- Dube msimu huu amefanikiwa kumaliza kwa kuifungia Yanga mabao 10 akizidiwa mabao manne na kiungo Allan Okello aliyekuwa kinara ndani ya timu hiyo
Dar es Salaam. Mshambuliaji Prince Dube amepiga chini ofa tatu kubwa na kufanya uamuzi magumu ya kurejea nchini kwao Zimbabwe akisaini mkataba wa miaka miwili.
Dube amesaini mkataba na Hardrock ya kwao Zimbabwe baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga mwisho wa msimu huu.
Mshambuliaji huyo awali Yanga ilimuwekea ofa kubwa mezani ya kuongeza mkataba akakubali lakini baadaye akabadili mawazo akitaka kutafakari upya.
Dakika chache zilizopita Hardrock imemtambulisha mshambuliaji huyo kuwa mchezaji wao mpya baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika.
Kabla ya kukubali ofa ya Hardrock, Dube alipokea ofa kubwa ya Sh1 bilioni kusaini Al Ittihad ya Libya lakini mshambuliaji huyo akaigomea.
Ofa nyingine kubwa ni ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambayo ilitaka kumpa kiasi cha Sh950 milioni lakini nayo akaigomea.
Dube msimu huu amefanikiwa kumaliza kwa kuifungia Yanga mabao 10 akizidiwa mabao manne na kiungo Allan Okello aliyekuwa kinara ndani ya timu hiyo