Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

England, Argentina ilivyoingia kwenye mtego wa kisiasa

Kuelekea Kombe la Dunia 2026, Argentina walikuwa na kampeni yao ya La Quarta Estella yaani Nyota ya Nne.

Nyota ya nne maana yake ni ubingwa wa nne wa dunia kwa sababu mabingwa wa dunia huweka nyota moja juu ya nembo ya timu kwenye jezi zao.

Argentina ni mabingwa mara tatu wa dunia....kwa hiyo wana nyota tatu, walienda Amerika Kaskazini kuisaka nyota ya nne...La Quarta Estella.

Mwanamuziki mmoja mashuhuri nchini humo, Palmito, akatunga wimbo maalumu kuhanikiza kampeni hii...ukaitwa jina hilo hilo, La Quarta Estella.

Mashairi ya wimbo huu yamebeba ujumbe wenye hisia kali za ushabiki wa mpira lakini zaidi ni uzalendo na utaifa.

Moja ya mashairi yanayobeba hisia za uzalendo na utaifa ni yale yanayosema

Soy argento de la cuna hasta el cajón

-Mimi ni muargentina tangu kuzaliwa hadi kufa.

Por Malvinas,

-Kwa ajili ya Malvinas,

Por el Diego

-Kwa ajili ya Diego.

Por la ultima de Leo

-Kwa ajili ya ubingwa wa mwisho wa Leo


Hapa wanamaanisha kwamba wamekwenda kucheza Kombe la Dunia kwa ajili ya mambo makuu manne.

i. Kwa ajili ya kupata nyota ya nne

ii. Kwa ajili ya Malvinas

iii. Kwa ajili ya Diego (Maradona)

iv. Kwa ajili ya kumpa heshima ya mwisho Lionel Messi


NYOTA YA NNE

Kwa ajili ya nyota ya nne tumeshaona hapo juu.


KWA AJILI YA DIEGO

Diego anayetajwa hapa ni Maradona. Mashindano haya yanafanyika Marekani ambako mwaka 1994 Maradona aliondolewa kwenye mashindano kwa kukutwa akitumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni.

Lakini Argentina wanaamini lile lilikuwa zengwe kumzuia asishinde ubingwa.

Kwa hiyo wanaposema kwa ajili ya Diego, maana yake safari wameenda kumlipia kisasi.


KWA AJILI YA UBINGWA WA MWISHO KWA LEO

Leo anayetajwa hapa ni Messi...Lionel Messi.

Wanaamini kwamba haya ni mashindano yake ya mwisho kutokana na umri wake. Kwa hiyo lazima washinde ili kumuaga vizuri.


KWA AJILI YA MALVINAS

Hapa ndipo kwenye kimbembe.

Malvinas ni jina ambalo Argentina wanalitumia kuviita visiwa vya Falklands.

Hivi ni visiwa vilivyopo karibu kabisa na Argentina, lakini viko chini ya Uingereza.

Argentina wanaamini visiwa hivi ni vya kwao...na ndivyo wanavyoamini Uingereza pia.

Mataifa haya yameshawahi kuingia vitani mwaka 1982 kugombania visiwa hivi.... Argentina ikapigwa vibaya sana.

Mwaka 1986 kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia kati ya England na Argentina nchini Mexico, nahodha Maradona aliwaambia wachezaji kwamba wakashinde mechi ile ili kuwalipia kisasi askari wao waliouawa kwenye vita.


Na ndipo akafunga bao la mkono wa Mungu.

Inapokuja mechi ya England na Argentina, kitu cha kwanza kinachotangulia ni hii vita na siasa za visiwa vya Falklands au Malvinas, halafu mpira unafuata.

Wachezaji wa Argentina huuimba wimbo wa La Quarta Estella kila wanaposhinda mechi yao.

Lakini katika mara zote, hakuna siku waliimba kwa hisia kama waliposhinda mechi ya robo fainali dhidi ya Uswisi, na kujua kwamba watakutana na England kwenye nusu.

Hapa ilikuwa wanatuma ujumbe kwamba wataingia kwenye mechi hiyo kulipa kisasi cha 1982 na kuonesha hasira zao kwa waingereza.

Na hata siku ya mechi wakati wamejipanga kuimba wimbo wa taifa kabla ya mechi, hisia zilikuwa tofauti na wakati wowote.

Waliimba kwa uchungu mkubwa sana wakionesha kabisa wanakwenda kupigana vita...na hata mechi yenyewe waliicheza kivita.

Siasa za Argentina na England ni kubwa kiasi kwamba hata waamuzi wa England hawaruhusiwi kuchezesha mechi za Argentina.

Michael Oliver na Anthony Taylor ni waamuzi wa England wenye daraja la juu lakini waliondolewa kwenye orodha ya waamuzi kuanzia hatua ya nusu fainali kwa sababu ya siasa.

Ni kwamba nchi yao England ilifuzu hatua yao, na Argentina pia.

Wasingeweza kuchezesha mechi ya England lakini pia hawatakiwi kuchezesha mechi za Argentina.

Na hii ni hata kinyume chake, waamuzi wa Argentina Facundo Tello na Yael Falcon Perez pia waliondolewa.


NI MECHI ILIYOLETA KADI

Kabla ya England na Argentina kucheza mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia 1966, hakukuwa na kadi kwenye mpira.

Mchezaji akifanya makosa alikuwa aidha anaonywa tu kwa mdomo au anatolewa nje kwa kuambiwa tu mwamuzi...nenda nje!

Mwaka 1966 England na Argentina zilikutana kwenye robo fainali.

Dakika ya 35, mwamuzi Rudolf Kreitlein kutoka Ujerumani akamtoa nje nahodha wa Argentina, Antonio Rattin, ambaye amefariki Julai 11 mwaka huu.

Akamwambia kwa maneno atoke nje...jamaa hakutoka...akabaki uwanjani.

Akataka aletwe mkalimani ili amtafsirie maneno ya refa.

Jamaa kabisa kutoka hadi polisi wakaenda kumchukua na kumtoa nje.

Baada ya mashindano haya, mwamuzi wa England, Ken Aston, akatafuta suluhisho la utata wa lugha kama uliotokea kwenye Ile mechi.

Akapendekeza badala ya mwamuzi kumwambia kwa maneno mchezaji atoke, kuwe na kitu ambacho watu wote watakijua na kuelewa kwamba kina maana ya mchezaji kuonywa au kutolewa.

Ndipo akiwa kwenye mataa ya barabarani, likamjia wazo la kutumia rangi za taa.

Njano kama onyo....kama ilivyo barabarani, na nyekundu kama hatari.

Wazo hili likakubaliwa na FIFA na kuanzia 1970 kadi zikaanza kutumika.

Kwa hiyo bila utata wa Antonio Rattin dhidi ya mwamuzi Rudolf Kreitlein kwenye mechi ya England na Argentina, yawezekana kadi zisingekuwepo.