Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fainali ya rekodi CHAN 2024, Morocco ikitwaa ubingwa

Muktasari:

Fainali za CHAN zilianzishwa mwaka 2009 zikishirikisha wachezaji wanaocheza katika Ligi za Ndani za mataifa shiriki.

Rekodi mbili zimeandikwa na fainali ya mashindano ya CHAN 2024 yaliyofikia tamati leo katika Uwanja wa Moi Kasarani, Kenya ambayo imemalizika kwa Morocco kutwaa ubingwa kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Madagascar.

Idadi ya mabao matano yaliyofungwa katika mchezo huo, yamefanya iwe mechi ya fainali ya mashindano ya CHAN ambayo imekuwa na idadi kubwa zaidi ya mabao ikivunja ile ya mwaka 2018.

Katika fainali ya 2018, mabao manne yalipachikwa katika ushindi wa mabao 4-0 ambao Morocco iliupata dhidi ya Nigeria na kutwaa ubingwa wa kwanza wa mashindano hayo.

Rekodi ya pili imewekwa na Morocco ya kuwa timu iliyotwaa mara nyingi zaidi ubingwa wa mashindano hayo ambapo imechukua kwa mara ya tatu na kuipiku ya mwanzo ambayo ilikuwa inaishikilia sambamba na DR Congo ya kutwaa ubingwa wa mashindano hayo mara mbili.

Mabao yaliyoipa ushindi Morocco katika mchezo wa leo yalipachikwa na Oussama Lamlioui ambaye alifunga mawili na lingine moja likiwekwa kimiani na Youssef Mehri huku yale ya Madagascar yakifungwa na Felicite Manohantsoa na Toky Rakotondraibe.

Kutwaa taji la CHAN 2024 kumeifanya Morocco ijihakikishie kitita cha Dola 3.5 milioni (Sh8.8 bilioni) ambacho kinatoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwenda kwa timu bingwa.

Madagascar ambayo imeshika nafasi ya pili, imejihakikishia kitita cha Dola 1.2 milioni (Sh3 bilioni).

Timu iliyomaliza katika nafasi ya tatu kwenye mashindano hayo ni Senegal ambayo awamu iliyopita ya 2022 ndio ilitwaa ubingwa.

Morocco haijatawala kama tu bali pia baadhi ya nyota wake wamefanikiwa kutwaa tuzo tofauti za wachezaji waliofanya vizuri ambapo Mchezaji Bora wa Mashindano hayo amekuwa ni kiungo wao Mohamed Hrimat.

Kwa mabao mawili ambayo Lamlioui amefunga leo, nyota huyo anayechezea RS Berkane amejihakikishia tuzo ya Mfungaji Bora wa mashindano hayo mwaka huu akimaliza akiwa amefumania nyavu mara sita.

Lamlioui amefuata nyayo za Wamorocco wenzake,  Ayoub El Kaabi aliyekuwa Mfungaji Bora wa Fainali za 2018 ambazo alifunga mabao tisa na Soufiane Rahimi ambaye katika Fainali za 2020 alipachika mabao matano na kuongoza chati ya kufumania nyavu.

Senegal ilipata tuzo ya Timu yenye Nidhamu na Mlinda Mlango wake Marc Diouf ameibuka mshindi wa tuzo ya Kipa Bora wa Mashindano.