Gamondi achonganisha washambuliaji Taifa Stars
Muktasari:
- Pia kuna Miano Danilo, Alphonce Mabula, Nathaniel Chilambo, Said Khamis, Suleiman Mwalimu, Yahya Zaydi, Offen Chikola, Jackson Kasanzu, Kibu Denis, Israel Mwenda, Kelvin John, Sabri Kondo, Nickson Kibabage, Paul Peter na Abel Josiah.
Dar es Salaam. Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Miguel Gamondi, amechochea vita ya mastraika na mabeki katika kuwania nafasi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Mataifa Afrika (AFCON) 2025 huko Morocco baada ya kuita kundi kubwa la wachezaji wa nafasi hizo katika kikosi chake cha awali.
Katika kikosi cha wachezaji 53 ambao Gamondi amewaita ambao watapunguzwa na kubakia 28 watakaoshiriki AFCON 2025, namba kubwa ni ya washambuliaji, ikifuatiwa na mabeki tofauti na viungo na makipa ambao hajaitwa wengi.
Kuna washambuliaji 19 ambao wameitwa ikiwa ni sawa na asilimia 35.8 ya kikosi kizima huku mabeki wakiwa ni 18 sawa na asilimia 34 na viungo wakiwa ni 11 ambao ni sawa na asilimia 20.8, wakati huo makipa wakiwa wanne ambao ni asilimia 7.5 tu.
Kwa washambuliaji, Gamondi amewarudisha kundini Saimon Msuva, Said Khamis, Nassor Saadun, Athuman Makambo, Mbwana Samatta, Iddi Kipagwile, Vitalis Mayanga,Cypprian Kachwele na Kibu Denis ambao hakuwaita katika kikosi chake kilichopita.
Licha ya kutopata nafasi katika kikosi cha Simba, beki Vedastus Masinde amejumuishwa kikosini huku pia akiwemo nyota wa timu ya vijana chini ya miaka 20 ya JKT Tanzania, Abel Josiah.
Kikosi hicho cha Taifa Stars, kinatarajiwa kuweka kambi nchini Misri kuanzia Desemba 7, mwaka huu kujiandaa na Fainali za Afcon ambazo zitafanyika kuanzia Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026.
Wachezaji 53 wanaounda kikosi cha awali cha Taifa Stars ni Hussein Masalanga, Yakoub Suleiman, Yona Amosi, Zuberi Foba, Haji Mnoga, Iddi Selemani, Ibrahim Abdullah, Dickson Job, Feisal Salum, Cyprian Kachwele, Ahmed Pipino, Abdul Suleiman na Mbwana Samatta.
Wengine ni Morice Abraham, Pascal Msindo, Wilson Nangu, Mohamed Hussein, Lusajo Mwaikenda, Mukrim Abdallah, Nassor Saadun, Elias Lawi, Yusuph Kagoma, Shomari Kapombe, Mudathir Yahya, Saimon Msuva, Athuman Makambo, Vedastus Masinde, Bakari Mwamnyeto, Novatus Miroshi, Tarryn Allarakhia, Charles M'mombwa, Iddi Kipagwile, Vitalis Mayanga, Khalid Habibu na Edwin Balua.
Pia kuna Miano Danilo, Alphonce Mabula, Nathaniel Chilambo, Said Khamis, Suleiman Mwalimu, Yahya Zaydi, Offen Chikola, Jackson Kasanzu, Kibu Denis, Israel Mwenda, Kelvin John, Sabri Kondo, Nickson Kibabage, Paul Peter na Abel Josiah.