Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Garnacho mbioni kujiunga Chelsea

Muktasari:

  • Chelsea pia ipo kwenye mazungumzo na RB Leipzig kuhusu uwezekano wa dili la kubadilishana wachezaji likihusisha Xavi Simons na Christopher Nkunku.

London, England. Winga wa Manchester United, Alejandro Garnacho, ameweka wazi msimamo wake kuhusu mustakabali wake huku akihusishwa na mpango wa kujiunga na Chelsea.

Mchezaji huyo wa Argentina, ambaye alijikuta kwenye orodha ya wachezaji watano waliotengwa na kocha Ruben Amorim mapema kiangazi sambamba na Jadon Sancho, Antony, Marcus Rashford na Tyrell Malacia anatafuta njia ya kuondoka Old Trafford ili kuepuka kukaa benchi msimu mzima.

Garnacho alielezwa mwezi Mei na Amorim kutafuta timu mpya, baada ya kuonyesha kutoridhishwa na kuanzia benchi kwenye fainali ya Europa League.

Kwa mujibu wa Daily Mail Sport, winga huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa anataka kuhamia Chelsea, klabu ambayo imeonyesha nia kubwa ya kumsajili. Awali United walikuwa wanataka pauni milioni 70 (Sh237 bilioni) lakini sasa wamepunguza bei hadi pauni milioni 50 (Sh170 bilioni) ili kuharakisha mauzo yake.

Inaelezwa kuwa Garnacho amewaambia mabosi wa United waandae uhamisho wake kwenda Chelsea kwani hayuko tayari kukaa benchi kwa miezi 6 hadi 12. Chelsea imeshaanza mazungumzo ya kina na United kuhusu dili hilo, huku tayari wakiwa wamekubaliana masharti binafsi na mchezaji.

Taarifa zinaeleza kuwa viongozi wa Chelsea hawana wasiwasi kuhusu tabia ya Garnacho baada ya kufanya uchunguzi wao, na mazungumzo kuhusu ada ya uhamisho yanaendelea.

Garnacho ameshacheza mechi 144 na kufunga mabao 26, akitoa pia pasi za mabao 22 akiwa na United. Ameshinda Kombe la FA msimu wa 2023/24 na Kombe la Carabao (EFL Cup) msimu uliotangulia.

Wakati huohuo, Chelsea pia ipo kwenye mazungumzo na RB Leipzig kuhusu uwezekano wa dili la kubadilishana wachezaji likihusisha Xavi Simons na Christopher Nkunku, ambaye aliwahi kupata mafanikio makubwa kwenye Bundesliga kabla ya kujiunga na The Blues.