Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sancho apewa njia ya kuondoka Man United, Roma, Besiktas zaingia vitani

Muktasari:

  • Rashford, ambaye pia alikuwa sehemu ya kundi la wachezaji waliotengwa, tayari amejiunga na Barcelona kwa mkopo wa msimu mzima.

Winga wa Manchester United, Jadon Sancho, anaweza kuondoka Old Trafford baada ya kuripotiwa kuwa vilabu viwili viko tayari kumpa hifadhi.

Sancho, Alejandro Garnacho, Antony na Tyrell Malacia wamekuwa wakifanya mazoezi nje ya kikosi cha kwanza tangu waliporipoti kwa maandalizi ya msimu mpya mwezi uliopita, na waliondolewa kwenye orodha ya wachezaji waliokwenda ziara ya Marekani. Marcus Rashford, ambaye pia alikuwa sehemu ya kundi la wachezaji waliotengwa, tayari amejiunga na Barcelona kwa mkopo wa msimu mzima.

Sancho amekuwa kwenye mazungumzo na Borussia Dortmund na Juventus majira haya ya kiangazi, lakini dili bado halijakamilika. Hali yake imekuwa tata zaidi baada ya Chelsea kuamua kulipa pauni milioni 5 ili kuvunja mkataba wa kumchukua kwa kudumu kwa pauni milioni 25.

Ripoti zinadai Dortmund haina uhakika wa kumsajili kwa mara ya tatu, huku Juventus ikichelewesha maamuzi ikisubiri kuuza baadhi ya wachezaji wake. Hata hivyo, AS Roma na Besiktas zimejitosa rasmi kwenye mbio za kumwania nyota huyo wa England.

Kwa mujibu wa Football Italia, Roma tayari imeanza mawasiliano na United kujua masharti ya dili hilo. Kocha mpya wa Roma, Gian Piero Gasperini, anadaiwa kumkubali sana Sancho, ingawa haijulikani kama mchezaji huyo atakubali kuhamia Italia.

Besiktas, inayofundishwa na aliyewahi kuwa kocha wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer, pia imeonyesha nia. Rais wa klabu hiyo, Serdal Adali, amesema angependa kumleta Sancho lakini changamoto kubwa ni mshahara wake mkubwa na ukosefu wa ushiriki wa Ligi ya Mabingwa.

“Kadiri jamii ya mashabiki wetu inavyomtaka, mimi pia nataka. Lakini si suala la matakwa yetu pekee, bali pia kama mchezaji mwenyewe yuko tayari kuja Uturuki. Tuna bajeti yetu, tutafanya kila jitihada, lakini wachezaji kama Sancho mara nyingi hupendelea vilabu vya Ligi ya Mabingwa,” amesema Adali akizungumza na Turkiye Today.

Sancho, mwenye umri wa miaka 25, amebakisha miezi 11 pekee kwenye mkataba wake huku akilipwa mshahara wa pauni 275,000 (Sh93 milioni) kwa wiki jambo linaloifanya United kufikiria tena mpango wa kumtoa kwa mkopo.

Mbali na Juventus na Roma, Inter Milan pia imeonesha nia, wakimchukulia kama mbadala wa Ademola Lookman iwapo Atalanta itakataa kumuuza mshambuliaji huyo.