GSM akomaa ishu ya kina Mayele, Djuma

GSM akomaa ishu ya kina Mayele, Djuma

Muktasari:

  • Kuanzia juzi zilipotoka taarifa za wachezaji wanne wa Yanga kuzuiwa CAF ambao ni Djuma Shaban, Fiston Mayele na Khalid Aucho, Bilionea wa Yanga Ghalib Said Mohammed ‘GSM’ baada ya kuambiwa umuhimu wa mastaa hao na Kocha Nesreddine Nabi akataka mawasiliano ya haraka yafanyike.

Dar es Salaam. Kuanzia juzi zilipotoka taarifa za wachezaji wanne wa Yanga kuzuiwa CAF ambao ni Djuma Shaban, Fiston Mayele na Khalid Aucho, Bilionea wa Yanga Ghalib Said Mohammed ‘GSM’ baada ya kuambiwa umuhimu wa mastaa hao na Kocha Nesreddine Nabi akataka mawasiliano ya haraka yafanyike.

Akili ya Ghalib anataka hata kama kwa kulipa faini yuko tayari kufanya hivyo ili Yanga iwapate mastaa hao ingawa bado wanapambana.

Ghalib alinunua mastaa hao pamoja na wengine wa kigeni wakiangalia zaidi mechi za kimataifa.