Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gumzo ndoa ya Hakimi, mkewe Abouk ikivunjika

Muktasari:

  • Aliyekuwa mke wa mchezaji wa Klabu ya PSG, Achraf Hakimi aitwaye Hiba Abouk baada ya kuachana na mumewe Machi 27, 2023  alienda makamani na kuwasilisha kesi ya kudai talaka huku akitaka agawiwe nusu ya mali.

Dar es Salaam. Aliyekuwa mke wa mchezaji wa Klabu ya PSG, Achraf Hakimi aitwaye Hiba Abouk baada ya kuachana na mumewe Machi 27, 2023  alienda makamani na kuwasilisha kesi ya kudai talaka huku akitaka agawiwe nusu ya mali.

Baada ya Mahakama kufanya tathmini ya mali za Hakimi ilibaini kuwa hamiliki chochote kwani vyote anavyomiliki vimesajiliwa kwa jina la mama yake mzazi.

Hakimi analipwa mshahara wa Euro 1 milioni kwa mwezi ikiwa ni zaidi ya Sh2.56 bilioni ndani ya PSG lakini asilimia 80 ya mshahara huo huwekwa kwenye akaunti ya mama yake, Fatima.

"Hana mali, magari, nyumba, vito au hata nguo kwa jina lake. Wakati wowote na akitaka chochote huwa anaulizia kwa mama yake ambaye huwa anamnunulia," ilisema taarifa ya mahakama.

Abouk (36), alipompeleka mumewe mwenye umri wa miaka 24 mahakamani, alitarajia kupata mgawo sawa wa Euro 70 milioni baada ya kutengana, lakini aliarifiwa kwamba nyaraka zilionyesha mali zake zote ni za mama yake.